Breaking News

JESHI LA POLISI LIMEWAKAMATA MAJAMBAZI WATATU JIJINI DAR

Timothy Marko
Jeshi la polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limefanikiwa kuwakamata watuhumiwa watatu wa ujambazi waliofanya tukio la unyang'anyi wa kutumia silaha kwa wakala wa kutoa na kuweka fedha siku ya tarehe 26 Jan 2022 Maeneo ya Mbagala zakhem jijini Dar es salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Kamanda wa kanda Maalum, ACP Muliro Jumanne Muliro amemtaja mmoja ya mtuhumiwa Mrisho maarufu kama Bonge pamoja wenzake wawili ambao majina Yao yamehifadhiwa.

"Watuhumiwa wamehusika katika tukio lililotokea tarehe 26 January majira ya saa mbili usiku huko Mbagala zakhemu  Karibu na Duka la Rosemary Kimario ambaye ni wakala na mtoa huduma za kuweka na kutoa kifedha katika motandao mbalimbali". Alisema Kamanda Muliro.

Alisema majambazi walikuwa na Pikipiki yenye namba za usajili MC 908 DBG Aina ya HOAJUE ambapo wakati wa tukio askari walifika eneo la tukio na baada ya kutambua walianza kurusha risasi ambapo askari Polisi walijihami na  kujibu mashambulizi kwa wahalifu hao .

"Watuhumiwa walifika eneo la tukio wakiwa na bastora modeli 75 CAL PARA yenye no. K 4596 ikiwa yenye Magazine moja na risasi kumi na moja kwa lengo la kufanya uhalifu".

Kamanda Muliro Aliongeza kuwa sambamba na silaha hiyo pia majambazi hao walikutwa na noti bandia za kitanzania zenye thamani zaidi ya Tsh Milioni 1.8 ambazo huzitumia kama njia pindi wanapotaka kufanya tukio la uhalifu kwa kujifanya wanataka kuweka fedha na kisha kuwa pora Fedha.

Aidha Jeshi la polisi limeendelea kutoa wito kwa wananchi na raia wema kuendelea kutoa taarifa kwa jeshi hilo pindi wanapogundua tukio la uhalifu hata viashiria vya kufanyika kwa uhalifu au mpango wa  hili kuzuia vitendo hivyo.

No comments