Breaking News

MSUYA: WASANII WA NYIMBO ZA INJILI NA WAIGIZAJI JIUNGENI NA CHAMA KUWEZA KUTETEA MASLAHI YENU

Wasanii na waigizaji nchini wametakiwa kujiunga na chama cha wasanii wa nyimbo za injili na utangazaji hili kuweza kunufaika na fursa mbalimbali zinazopatikana katika chama hicho

Akizungumza jijini Dar es salaam na Mwenyekiti wa Mtandao huo Bw. David Msuya amesema lengo kubwa la kuanzishwa kwa mtandao huo ni kuwaunganisha wasanii wa nyimbo za Injili na wagizaji pamoja kuweza kuwa na sauti moja. 

"Lengo kuu la kuanzishwa kwa mtandao wa wasanii wa injili na waigizaji ni kuwaunganisha wasani na wadau pamoja, kutatua changamoto wanazo kabiliana nazo" alisema Bw. Msuya

Alisema mtandao wa wasanii wa nyimbo za Injili na waigizaji tanzania ni wa kizalendo na upo kushirikiana na serikali katika kuhakikisha adhama yake ya kuhhakikisha wasanii wananufahika na kazi zao inafikiwa.

Bw Msuya aliongeza kuwa katika kuhakikisha adhima hiyo ya serikali ya awamu ya sita inafikiwa hiyo kuwawezesha wasanii na wanachama wa mtandao huo kuweza kunufaika na kazi zao

No comments