Breaking News

WAZIRI UMMY: SERIKALI YATENGA FUNGU KATIKA MAPATO MAEGESHO KUBORESHA MIUNDOMBINU NA KUKARABATI BARABARA

Serikali imesema katika Fedha zitakazo kusanywa katika ushuru wa maegesho zinatarajiwa kuboresha Miundombinu ya Barabara sambamba ukarabati wa taa za Barabarani.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wahabari jijini Dar es salaam Waziri wa Tawala  za mikoa na serikali za mitaa (Tamisemi) mhe. Ummy Mwalimu amesema katika kuwa katika kipindi cha 2020/21 jumla ya milioni 45 zilikusanywa Kwa Mwaka 2021 ambapo mwaka jana ilikusanya mil 25.

"katika kipindi kijacho cha Mwaka wa Fedha 2022/23 ushuru unaotokana na wa Magari, Fedha hizi asilimia 40 zitapelekwa  Katika Halimashauri za jiji  ambapo Fedha hizo zitatumika kutanya usafi wa Barabara, ukarabati mifereji, uwekaji wa taa za barabarani Sambamba upandaji wa Maua"Alisema Waziri Ummy Mwalimu.

Waziri Ummy Alisema kumekuwa na tabia zisizofaa Kwa Baadhi ya watumishi wanaotoa lugha za matusi wakati wa ukusanyaji mapato ya maegesho amewataka kuacha tabia hizo na atayebainika atachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kufukuzwa kazi.

Katika hatua nyingine Waziri Ummy ameongeza kuwa ifikapo  Desemba Mosi Mwaka huu makusanyo yote yatafanyika kieletroniki.

No comments