DR. POSS ASHIRIKI MAONYESHO YA KUKUZA VIPAJI JIJINI DAR
kaimu katibu mkuu wa wizara ya sanaa utamaduni na michezo, Dr. Ally Poss amesema serikali itaendelea kuboresha na kuweka mazingira mazuri ya lengo la kukuza Sanaa na Uchoraji kuiwezesha kuwa ni moja ya fursa ya kukuza uchumi.
Akizingumza wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya kumi ambayo yameandaliwa na East Africa Art Biennale Association ( EASTAFAB) yanayofanyika katika kituo cha nafasi art space jijini dar es salaam.
Alisema Sanaa ya Uchoraji ni muhimu kwa Jamii pamoja na kutoa elimu, kuburudisha serikali itahakikisha inaweka mazingira bora kuhakikisha Sanaa ya Uchoraji iwe fursa ya uchumi kwa Taifa
"Serikali inatambua mchango wa Sanaa ya Uchoraji na Sanaa zingine tutaendelea kuboreshea mazingira ili wasanii wetu tumeanzisha mfuko ambao utasaidia kutoa mikopo ya riba nafuu ili kuwainua wasanii wetu waweze kunufaika na vipaji vyao". Alisema Dr. Poss.
Kwa upande wake Mwanzilishi wa maonyesho hayo ya East Africa Art Biennale Association ( EASTAFAB), Prof. Elias Jengo amesema maonyesho ya mwaka huu yatafanyika kwa siku 20 na kazi mbali mbali za sanaa ya uchoraji zitaonyeshwa.
"Maonyesho ya mwaka huu yatafanyika kwa siku 20, kazi mbalimbali za sanaa ya uchoraji zitaonyeshwa katika kipindi chote cha maonyesho hayo kwa lengo la kukuza na kuinua sanaa ya uchoraji nchini."
Alisema katika maonyesho hayo kutakua pia na kongamano ambalo litawashirikisha wasanii wote ili watoe mawazo yao yatakayosaidia kuinua Sanaa zetu, tutakua na maazimio ambayo tutayawasilisha kwenu serikali muweze kuyafanyia kazi" amesema Prof. Jengo.
Nae Mkurugenzi wa kituo Cha Nafasi Arts Space, Bi. Rebecca Yeing Ae Mzengi Corey amesema kituo hicho kitaendelea kuibua vipaji na kuviendeleza ili vijana wengi waweze kujiajiri kupitia vipaji vyao.
Mwakilishi wa Balozi wa Norwey Annete Otilie amepongeza kuwepo kwa usawa wa kijinsia wanawake wamekuwa wakipewa nafasi ya kushiriki katika mambo mbalimbali ya Sanaa huku akisisitiza kuwa Norwey itaendelea kusaidia kituo hicho katika kukuza Sanaa.
"Tanzania imepiga hatua kuwa katika swala la usawa wa kijinsia kwa kuzinhagita usawa hususani katika nyanja za michezo"
Katika Tamasha la mwaka huu washirki kutoka mataifa mbalimbali kutoka Tanzania, Kenya, Uganda waameahiriki katika tamasha hilo la kumi na moja.
No comments