Breaking News

“CHANGAMOTO HAZIKOSEKANI LAKINI LAZIMA MIJI IPANGWE" WAZIRI UMMY

Nteghenjwa Hosseah, Dar es salaam
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amesema changamoto hazikosekani lakini Miji yetu ni lazima ipangwe sambamba na kuwapelekea wafanyabiashara katika maeneo yaliyoandaliwa ili kufanya biashara kwenye mazingira bora. 

Waziri Ummy ameyasema hayo alipotembelea  Soko la Karikaoo kuangalia maandalizi ya ukarabati wa Soko la zamani sambamba na ujenzi soko Jipya la Kariakoo.

“Nimefika leo kwa ajili ya kufatilia na kutekelezeka maelekezo ya Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kuhusu Soko la Kariakoo.

Lazima miji ipangwe, na tunamshukuru Mhe. Rais amesisitiza lazima miji ipangwe na iwe salama, changamoto hazikosekani lakini tuzitatue naupongeza Mkoa wa Dar es Salaam kwa jitihada kubwa za kuwapanga wamachinga. 
Naelekeza Fedha zilizotolewa na Mhe. Rais Shilingi. Bil 32.2 ziombwe na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam sababu mradi huu ni mkubwa na Wilaya watakua wafuatiliaji wa karibu lakini Mkoa lazima wasimamie kikamilifu.

“Ninachotaka kuona ni Soko lijengwe kwanza baadae ndo tutajua namna ya Menejimenti kama lisimamiwe na Jiji au Shirika la Masoko Kariakoo. 

Soko letu liliungua July, tulipeleka maombi kwa Mhe. Rais ya kulikarabati ametukubalia, na ametukubalia kujenga soko lingine kubwa litakuwa na Ghorofa sita kwenda juu na mbili kwenda Chini”.
Aidha ameagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es salaa kuomba fedha hizo wizara ya Fedha na Mipanho si zaidi ya tarehe 15 mwezi huu ili kazi ianze mara moja, uanze ukarabati wa soko hili na ujenzi wa soko lingine jipya.

“Soko Jipya litakuwa na wafanyabiashara zaidi ya elfu 2,vipaumbele ni hivyo wala wafanyabiashara wasiwe na wasiwasi wote watapewa maeneo ya biashara naada ya ukarabati na ujenzi".

 

No comments