Breaking News

WAZIRI UMMY AMPONGEZA RC MAKALLA KWA KURATIBU VIZURI ZOEZI LA KUWAPANGA MACHINGA

Waziri wa Nchi ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Ummy Mwalimu amepongeza Mkoa wa Dar es salaam kupitia Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Amos Makalla kwa kuratibu vizuri zoezi la kuwapanga Machinga pasipo uvunjifu wa amani na Sasa taswira ya Jiji imeanza kurudi.

Waziri Ummy ametoa pongezi hizo wakati wa ziara ya kutembelea Soko la Kariakoo lililoungua ambapo amesema lazima ifikie mahala Miji iwe Katika mpangilio mzuri
 ili kulinda taswira ya miji na Majiji.
Aidha Waziri Ummy amesema hivi karibuni anatarajia kufanya kikao kazi na Maafisa Mipango Miji ili kuweka mikakati thabiti ya kuboresha majiji.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla amesema kwa Sasa Mkazo Serikali ya Mkoa huo ni kuendelea kufanyia maboresho changamoto zote zitakazoonekana kwenye maeneo walipopelekwa Machinga ili wafanye Biashara zao bila usumbufu.


No comments