Breaking News

REGINA KIHWELE (GYNAH) ANYAKUA TUZO YA MUIGIZAJI BORA NCHINI KENYA.. BODI YA FILAMU YAMPONGEZA.

Bodi ya Filamu Tanzania inaungana na Wanatsnia wa Filamu nchini kumpongeza Muigizaji wa Filamu ya MULASI kutoka Tanzania Bi. Regina Kihwele almaaruf Gynah, kufuatia kushinda Tuzo ya Muigizaji bora wa kike katika mashindano ya Tuzo za Lake International Panafrican Film Festival (LIPFF), ambapo kilele chake kilifanyika Tarehe 6/11/2021, Nairobi nchini Kenya.

Tuzo hizo zimejikita katika kutazama Filamu zenye maudhui ya Kiafrika, ambapo Filamu ya Mulasi imebeba maudhui yanayoonesha vivutio vya Utalii vinavyopatikana nchini katika mandhari ya kijijini katika Mkoa wa Dodoma.
Katika Kipengele ambacho Bi. Regina ameshinda alikuwa akishindana pamoja na Washiriki wengine kutoka nchi za Afrika Kusini, Kameruni, Moroko na Uganda, ambapo yeye kutoka Tanzania ameibuka mshindi.

Aidha, katika kuunga mkono jitihada za Wanatasnia ya Filamu nchini, Tarehe 28.10.2021 Bodi ya Filamu ilimuaga na kumtakia kila la heri kwa kumkabidhi Bendera ya Taifa Muigizaji huyo Bi. Regina, ili akawe Balozi wakuitangaza Tanzania Kimataifa.
Bi. Regina katika siku hiyo alikabidhiwa bendera pamoja na Watayarishaji wa Filamu ya Nyara iliyochaguliwa kuingia kwenye kipengele cha Filamu Bora Ndefu, na Muigizaji Bora kupitia Bw. Cojack Chilo, ambapo wote walichaguliwa kuwania Tuzo.

 

No comments