Breaking News

CAGBV WAENDESHA ZOEZI LA UPIMAJI VVU KWA HIARI PAMOJA NA KUTOA ELIMU YA UNYANYASAJI WA KIJINSIA

Kufuatia kuelekea kilele cha  maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani inayoazimishwa Desemba Mosi kila Mwaka, Kituo cha Kupinga Unyanyasaji na ukatili wa Kijinsia (CAGBV) kimefanya zoezi la utoaji wa elimu kuhusu upimaji wa ukimwi.

Zoezi hilo ambalo limefanyika katika viwanja vya ofisi za shirika hilo jijini Dar es salaam, kwa kushirikiana na halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wametoa elimu kwa wananchi pamoja na kushiriki upimaji wa hiari wa VVU na Ukimwi.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Mwamasishaji na mtoa elimu ya maswala ya kijinsia (CAGBV), Bi Kanisia Komba amesema shirika wamekua limekuwa mstari wa mbele kwa kushirikiana na wadau wengine ikiwemo serikali kutoa elimu kuhusu maswala mbalimbali ikiwemo kuwaelimisha wanawake kutambua haki zao, kujiamini, kiuchumi pamoja namna ya kukabiliana ukatili wa kijinsia.

"Leo Taasisi yetu kwa kushirikiana na halmashauri ya Ubungo na wadau wengine katika kuelekekea kilele cha siku ya Ukimwi duniani tumeamua na kutoa elimu kwa makundi mbalimbali kutambua umuhimu wa kupima na kujua afya zao, pamoja na kutoa elimu juu ya mabukizi ya Ukimwi, Magonjwa ya zinaaa pamoja na namna ya kuzuia ukatili wa kijinsia kwa jamii". Amesema Bi. Komba.
Kwa upande wake  Mratibu wa Vijana wa Shirika hilo Bw. Kassim Abdalah ametoa wito kwa jamii hususani vijana kutambua kwamba Ugonjwa hatari wa Ukimwi upo na wachukue tahadhari.

"Kwa mujibu wa takwimu kundi la vijana ndio kundi ambalo ni hatari zaidi hivyo napenda kutoa wito kwa jamii hasa vijana kushiriki kupata elimu ya kujitambua na namna ambavyo wanaweza kujikinga na ugonjwa huo, mimba zisizotarajiwa pamoja na magonjwa ya zinaa" Alisema Bw. Abdalah

Alisema shirika pamoja na changamoto mbalimbali katika utendaji wao kazi katika jamii hususani kwa jamii inayotendewa ukatili wa kijinsia kwa kuchelewa au kushindwa kutoa taarifa za matukio hayo kwa kuogopa jamii, lakini kwa kushirikiana na serikali pamoja na wadau wengine wamekuwa wakianzisha madawati ya kijinsia kutoa elimu kwa jamii katika maeneo mbalimbali.

"Shirika kwa kushirikiana na wadau wengine wamekuwa wakikumbwa na changamoto mbalimbali katika utendaji wao kazi hasa katika jamii inayotendewa ukatili wa kijinsia kama vile kushindwa au kutotoa taarifa kwa kuogopa jamii".

No comments