Breaking News

MADERAVA BAJAJI ULEMAVU DAR WAJA NA OMBI HILI KWA RC MAKALA

Umoja wa madereva wa bajaji walemavu mkoa wa Dar es salaam (UWAWABADA) umemuomba mkuu wa mkoa wa Dar es slaam kutoa kauli ya kuwarudisha kwenye maeneo yao ya awali ambayo walipangiwa kufanyabiabiashara ya bajaji.

Wito  huo umetolewa na mwenyikiti wa Umoja huo Dar es salaam Nyekoba Msabi  wakati wakati wakizungumza na vyombo vya habari juu ya masuala mbalimbali yanayowahusu walemavu hao ,ambapo wameomba waendesha bajaji wasio na ulemavu wasiluhusiwe kuingia katikati ya mji kama ilivyokua awali kabla ya mripuko wa kwanza wa ugonjwa uviko 19.

Bwana Msabi amesema waendesha bajaji wengi hali zao zimekua mbaya kutokana nakushindwa kufanya marejesho kutokana na bajaji walizokopeshwa huku wengine wakinyang'anywa bajaji hizo kutokana na tangazo la aliekua mkuu wa mkoa wa dar es salaam serikali ya awamu ya tano Paul Makonda kuruhusu waendesha bajaji wasio na ulemavu kuingia katikati ya jiji.

"Bajaji tunazoendesha tumezikopa manispaa, zingine tumekopeshwa na mhindi msamaria mwema bila riba hivyo tumeshindwa kurejesha kwa wakati marejesho yetu hadi wengine bajaji wamenyang'anywa hivyo tunamuomba mkuu wa mkoa Amosi Makala utusaidie kutoa tamko la kukataza waendesha bajaji wasio na ulemavu kuingia katikatibya mji manake hatuna uwezo wa kupambana nao katika ushindani wa wa kibiashara kupitia usafiri huo" amesema Msabi.
Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara walemavu Dar es salaam( UWAWADA) Juma Maleche ameushukuru uongozi wa Mkoa chini ya RC Makala kuwapangia sehemu nzuri na rafiki kwa watu wenye ulemavu kufanyabiashara nakuendelea kumsihi ahakikishe na masoko yote yaonyeshe sehemu za wafanyabiashara walemavu kabla ya kufunguliwa tena.

Aidha katika hatua nyingine mwenyekiti huyo ameuomba uongozi wa mkoa kuwadhibiti baadhi ya wafanyabiashara ambao wamekua wakirudi kwa nyakati za jioni katika maeneo yalioyopigwa marufuku kufanyabiashara.
Nae Doroth Mgimba ambaye ni mwenye ulemavu  amesema kwamba wamekua wakipitia changamoto mbalimbali,hivyo serikali iangalie namna ya kuendelea kuwapatia fursa hiyo kwa kuwaondolea vikwazo katika kufanya biashara.

No comments