Breaking News

UTOUH ASHAURI MAPENDEKEZO YA CAG KUFANYIWA KAZI

Na: Timothy Marko 
Mdhibuti na Mkaguzi mkuu wa Serikali mstaafu Ludovic utouh amewataka watendaji wa Serikali kutekeleza mapendekezo yanayotolewa na CAG ili kuboresha usimamizi wa Rasilimali za Taifa.

Akizungumza katika uzinduzi wa kitabu cha ukaguzi wa umma kiitwacho Misingi ya ukauguzi wa umma (principle Public  Sector Auditing) amesema kuzinduliwa Kwa Ripoti hiyo kutawasaidia  wananchi kuweza kuelewa namna ya Rasilimali zao zinavyo tumika katika kuwaletea maendeleo.

"Ripoti hii inaweza kutumika kama chanzo cha taarifa katika ufuatiliaji wa matumizi na Rasmali za umma kuanzia ngazi ya halmashauri "Alisema Mkaguzi mstaafu utouh.

Alisema Ripoti hiyo inafafanua umuhimu wa ukaguzi na maoni ya ukaguzi pamoja na Mambo nane ambayo Serikali inatakiwa kuyafanyiakazi.

Ameyataja mambo hayo ni pamoja na mwendo wa Hati za ukaguzi, mwendo wa utekelezaji wa mapendekezo ya CAG sambamba na maagizo ya kamati ya kudumu ya bunge  ya usimamizi wa Serikali za Mitaa.

"Ripoti hii imeandaliwa na taasisi ya wajibu Kwa ufadhili shirika la Maendeleo la ujerumani nchini Tanzania (GIZ) kupitia Mradi wa usimamizi Bora wa Fedha za Umma (GFG)." Aliongeza uttoh.

 

No comments