Breaking News

Waziri MULAMULA Ashiriki Maadhimisho Miaka 59 ya Uhuru wa Uganda

Timothy Marko
Katika Kuhakikisha Uchumi wa kikanda baina ya nchi wanachama wa jumuia ya Afrika Mashariki, Tanzania imesema itaendelea kushirikiana na nchi ya Uganda kama mwanachama wa jumuia hiyo katika Nyanja kiuchumi, kibishara, pamoja na uwekezaji.

Akizungumza katika Maadhimisho ya miaka 59 ya Uhuru wa nchi ya Uganda Waziri wa Mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema mahusiano ya nchi ya Uganda na Tanzania ya kindugu tangu enzi za Mwalimu Nyerere.

"Undugu wetu kati ya Tanzania na Uganda ni wa mda mrefu hivyo Tunu yetu ya Amani ni tunu ya maendeleo katika jumuhia yetu". Alisema Waziri Liberata Mulamula.

Kwa upande wake balozi wa Uganda hapa nchini, Richard kabonero alisema Safari miaka 59 ni kipindi kirefu katika kupigania Uhuru.

Alisema Tanzania inayo hifadhi ya Dola 800 milion ambapo hadi sasa na ina takribani makampuni 750 ambayo ni ya kitanzania.

No comments