VIJANA WENYE UMRI WA MIAKA 5 HADI 29 WAHANGA WA AJALI - Dk. MUHAMUZI
Timothy Marko.
Imelezwa wahanga wa ajali katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania ni vijana na watoto wenye umri Kati ya miaka mitano hadi miaka ishirini na Tisa.
Akizungumza katika Kongamano la kuwajengea uwezo wanahabari la kuhusiana na usalama Barabarani jijini Dar es Salaam Daktari wa taasisi ya mifupa (MOI) Dk. Bita Muhamuzi amesema katika nchi zinazoendelea idadi ya vifo vitokanavyo na ajali ni Asilimia 13 huku Magari yenye vidhibiti mwendo ni Asilimia moja wakati katika nchi zilizoendelea ni Asilimia Saba ndio inavidhibiti mwendo .
"Vijana na watoto waliokati ya miaka mitano Hadi miaka 29 ndio wahanga waajali ambao ninguvu kazi ya Taifa". Alisema Dk.Bita Muhamuzi.
Dk.Muhamuzi alisema vifo vinavyo tokana na ajali za Barabarani vimezidi ikilinganisha na Magonjwa ya TB na ukimwi.
Alisema Serikali zote Duniani zimeadhimia kupunguza vifo vitokanavyo na ajali Kwa asilimi50 ifikapo 2030.
"Shirika la afya Duniani WHO limebaini kuwa matumizi ya vilevi kutotumia vizuizi Kwa watoto kwenye Magari na kuendesha mwendokasi ndio chanzo kikubwa cha ajali nchini"Aliongeza Dk Muhamuzi.
Naye Muwakilishi wakikosi cha usalama Barabarani ASP Mussa Manyama aliwataka wadau wa usalama Barabarani ikiwemo waandishi wa Habari kuweza kutumia kalamu zao katika kuwaelimisha wananchi kuzingatia sheria za usalama Barabarani.
"Kumekuwa na usafiri wa bodaboda ambapo ajali nazozimekuwa zikiongezeka kutokana na kupuuza sheria za Barabarani hivyo niwajibu wenu Waandishi wa Habari kulielimisha kundi hili". Alisema ASP Mussa Manyama.

No comments