PRST Kufanya Mkutano Mkuu Oct 28 Jijini Dar
Bw Loth Makuza rais wa Chama cha Maafisa Uhusino wa Umma, (PRST), akifafanua jambo katika mkutano na waandishi (Hawapo pichani) jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Chama cha Maafisa Uhusino wa Umma (PRST), Bw. Ndege Makura akotoa ufafanuzi katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika hoteli ya Kebbys Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa kamati ya Maandalizi Bi Mary Kafyome akitoa maelezo kuhusu maandalizi ya mkutano huo.
Dar es Salaam:
Chama cha Maafisa Uhusino wa Umma,( PRST), kinataraji kufanya mkutano wake mkuu Oktoba 28 na 29, 2021 jijini Dar es Salaam ambao utawakutanisha wanachama wa chama hicho pamoja kutoka mikoa yote nchini.
Akizungumza na wandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Rais wa Chama cha Maafisa Uhusino wa Umma Tanzania (PRST), Bw Loth Makuza amesema maandalizi yote yamekamilika mgeni rasmi anataraji kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Jim Yonazi.
Alisema mkutano huo washiriki watapata wasaa kujadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na changamoto na mafanikio ya chama ambapo pia wadau wa watapata fusra ya kuijadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto hizo.
"Katika mkutano wetu wa siku mbili mada mbalimbali zitawasilishwa na kujadiliwa ikiwa ni pamoja na kujadili changamoto na mafanikio ya chama, pia wadau wa tasnia watashiriki kujadili na kuzichambua kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi" Alisema bw. Makuzi
Aidha bw Makuzi aliongeza kuwa mwaka huu pamoja na kuwakutanisha wanachama kutoka mikoa yote nchini pia Chama kinatarajia kupokea ugeni wa Marais wa vyama vya Maafisa Uhusino wa Umma katika nchi za Kenya na Afrika Kusini
“Hatujawahi kufanya mkutano mkubwa kama huu, huu ni mkutano wa watu wote waandishi wa habari, watu wa mahusiano, mawasiliano, masoko na TEHAMA, tutakuwa na mijadal mipana kuijadili taaluma na kuitetea”. Alisema
Mkutano huo pamoja na mambo mengine mwaka huu umewaalika wadau wote wa Habari, Mahusiano, Mawasiliano, Masoko na TEHAMA ambapo mada na mijadala mbalimbali itawasilishwa kwa lengo la kutatua changamoto zinazoikabili tasnia hiyo.
No comments