Breaking News

HALOPESA YAZINDUA HUDUMA YA PLAY & WIN, WATEJA KUZAWADIWA MAMILIONI

Kampuni ya Simu ya Halotel Tanzania kupitia huduma yake ya HaloPesa imezindua huduma ya “Play & Win” kwa wateja wake inayowapa fursa ya kujishindia zawadi kabambe.

Akizungumza na wanahabari leo jijini Dar es Salaam Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa HaloPesa Magesa Wandwi amesema Halopesa inakusudia kuwazawadia wateja wake mamilioni ya fedha na zawadi mbalimbali kila siku, wiki na kila mwezi kupitia michezo rahisi na shirikishi ya Play & Win iliyopo kwenye menyu ya HaloPesa kupitia *150*88#.

“HaloPesa zaidi ya kuwa tu huduma ya kifedha, sasa ni huduma Jumuishi ya kifedha na mtindo wa maisha kwa wateja wetu pamoja na kuwapa fursa wateja kuweza kununua muda wa maongezi kwa mitandao mingine na kupitia menyu ya Halopesa *150*88# unaweza kushiriki mchezo huu wa play &Win” amesema Magesa.

Amebainisha kuwa  uzinduzi wa huduma hiyo na Dunia Investment ni hatua nyingine ya ubunifu kutoka HaloPesa kufikisha thamani ya mtindo wa maisha kwa wateja wao.

Amebainisha kuwa  uzinduzi wa huduma hiyo na Dunia Investment ni hatua nyingine ya ubunifu kutoka HaloPesa kufikisha thamani ya mtindo wa maisha kwa wateja wao.

Amesisitiza kuwa Play & Win ni ubia wa kimkakati kati ya Dunia Investment na HaloPesa unaowezeshwa na Axieva Africa ambao umezindua aina mbalimbali za michezo ya kubahatisha nchini ikiwemo Tatu Dodo, Bid2Win, Win X-.

Ametoa wito kwa wateja wa Halotel kuendelea kucheza na kutumia huduma zao za HaloPesa na kujipatia fursa ya kujishindia pesa na zawadi mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkuu wa Huduma na Mahusiano kwa Wateja wa Dunia Investment, Kobus Schoeman amesema michezo na burudani ni sehemu asili ya utamaduni wa Kiafrika hivyo kila siku ni lazima mtu aiguse michezo na kwa sasa ni Play & Win kwa ushirikiano wa Halopesa.

Kobus amesema huduma hiyo kwa ushirikiano na HaloPesa inakusudia kuleta utamaduni huo kwenye simu ya mkononi na kwamba awe mteja asiye na ujuzi wa michezo ya bahati nasibu na mwenye shauku anayefahamu afurahie michezo hiyo hivyo mchezo huo ni wa wote na huduma hiyo inajumuisha watumiaji wa aina zote za simu na lugha ya kiswahili.

Amesema kuwa wanauhakika kuwa wateja zaidi wa Halopesa watafurahia huduma ya Play & Win na wale ambao bado hawatumii Halopesa wajiunge ili wafurahie huduma hiyo.

Nae, Afisa Bidhaa na Masoko wa Halo Pesa, Roxana Kadio amesema Sambamba na hayo kampeni ya Halopoints za Bure inalingana na aina ya miamala ambapo mteja atapewa Halopoints za Bure moja kwa moja wakati wowote anapofanya miamala ya HaloPesa ambapo pointi hizo anaweza kuzitumia kwenye michezo ya Play & Win.

 

No comments