Taasisi ya Mo Dewji Yatoa Mchango wa Mil 100 Kwa Kituo Cha Tumaini la Maisha
Wiki hii, Kwa mwaka wa 8 Taasisi ya Mo Dewji imetoa mchango katika kituo cha Tumaini La Maisha. Mwaka huu imechangia Millioni 100Tsh.
Dhamira ya kituo cha Tumaini la Maisha (TLM) ni kutoa matibabu ya bure yenye ubora wa juu kote Tanzania kwa kila mtoto ambae anasumbuliwa na saratani. Tumaini la Maisha ilianza kama kituo kimoja, na baadae iliongeza vituo 9 zaidi kote nchini.
Mwaka huu, mchango wa Millioni 100Tsh utasaidia katika upatikanaji wa dawa, huduma za shule, huduma za usafiri na shughuli nyingine mbalimbali. Tuna furaha kusaidia kituo cha Tumaini la Maisha katika kazi yake ya kuokoa maisha.
No comments