Breaking News

JATU PLC Yatangaza Kuuza Hisa Mil 15 na Kuingiza Bilioni 7.5

Kampuni ya kilimo na Biashara JATU PLC imetangaza matokeo ya hisa za milioni 15 ilizoziweka sokoni huku ikibainisha kuwa hisa hizo zimefanikiwa kuingiza  jumla ya kiasi cha Shilingi Bilioni 7.5.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Peter  Gasaya katika Mkutano Mkuu wa Wakulima wa JATU PLC uliofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Ubungo Plaza jijini humo.

Alisema kampuni imefanikiwa kuuza hisa milioni 155,263,372 na kupata Sh Bilioni 7.5 mabayo ni sawa na asilimia 104% ambapo malengo waliyojiwekea na kusisitiza kuvuka asilimia 4% ya walichokitegemea.

"Tuliingia soko la hisa tukauza hisa milion 15 kilichopatikana ni Sh bilioni 7.5 pesa ilienda kuwekeza kwenye Mradi wa Kilimo Kiteto mkoani Manyara kinachofanyika kwa umwagiliaji wa kisasa, msimu huu tunaongeza zao la ngano," alisema Gasaya.

Bw Gasaya aliongeza kuwa watu wasio Watanzania walionunua hisa hizo hawazidi watano na kwamba asilimia 99% walionunua hisa hizo ni wawekezaji watanzania na kusema wamepata wawekezaji wapya 10,000.

Amewashauri wakulima ambao hawajajiunga na kampuni hiyo kujiunga kwani mkulima akijiunga anapunguza gharama za ukulima katika hatua ya mwanzo hadi mavuno kwa kuwa JATU PLC wanamsimamia mwanachama hatua zote.
Amesisitiza kuwa katika matokeo yaliyotangazwa wakulima waliwekeza kwenye mazao mawili ya Mahindi na Mpunga ambapo mwaka 2019/20 wakulima kwa upande wa zao la mahindi walikuwa 71 na kwa mwaka 2020/21 waliongezeka kufikia 489 sawa na asilimia 589% huku jumla ya mavuno yalikuwa tani 9,509.58.

Ameongeza kuwa zao la mpunga kwa mwaka  2019/20 llilikuwa na wakulima 243 na 2020/21 walikuwa 599 sawa na 147% waliolima ekari 6,633 huku jumla ya tani 8,755.56 zilivunwa kwa mwaka huo.

Amewaomba watanzania kujiunga na JATU Saccos ili kuweza kukidhi vigezo vya kupata mikopo katika taasisi za fedha na kwamba kujiunga mwanachama anatakiwa awe na hisa angalau kwenye JATU PLC


No comments