Steve Nyerere: Mnaotumia Mitandao Kupotosha Juu Ya Chanjo Mkae Kimya
Na: Timothy Marko
Vijana ametakiwa kujitokeza kwa wingi kushiriki zoezi la chanjo ya virusi vya Corona 19 ambalo linaloratibiwa na wizara ya afya maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na watoto nchini.
Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam Msanii wa Maigizo nchini bw. Steve Nyerere alisema kumekuwa na minongo'no hususani katika mitandao ya kijamii kupotosha na kuamasisha watu kutopatiwa chanjo.
Kufatia kuongezeka kwa upotoshwaji huo ambao unawataka wananchi wasichanje chanjo Aina ya Johnson Johnson ni vyema wakaacha vitendo hivyo kwani Zoezi Hilo ni hiari ya mtu hivyo yawapasa kuwaacha watu kutumia Uhuru wao.
"Sisi tumeamua kuchanjwa wale wanao washwa washwa watakunwa tusitumie mitandao ya kijamii kuleta taharuki,"Alisema Steve Nyerere.
Alisema sisi wote mashahidi tangu kurpotiwa wimbi la tatu la ugonjwa huu wa Covid 19 duniani tukishuhudia vifo vingi vikitokea kwa nchi za wenzetu hii inatokana na kupuuza Zoezi Hilo.
Aliongeza kuwa Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassani amekuwa mfano mzuri katika kutekeleza Zoezi Hilo la chanjo ambapo yeye ka kiongozi amechukua hatua ya luchanjwa.
Naye Msanii wa Maigizo bwana Abdallah Mkumbila (Muhogo Mchungu) alisema kumekupo na upotoshwaji hasa katika mitandao kuhusu ugonjwa wa Corona, ugonjwa huo upo nilazima kuchukua tahadhari.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bendi ya Twanga Pepeta, Bi. Asha Baraka alisema yeye na Wasanii wenzake wapo tayari kuzunguka nchi nzima kwa ajili yakutoa Elimu ya kujikinga na Corona.
"Sisi kama wasanii ni kioo cha jamii hivyo tupo tayali kuzunguka nchi nzima kutoa elimu wa wananchi juu ya umuhimu na faida ya chanjo na kuhamasisha kuitikia wito mhe Rais Samia kuchanjwa japo ni kwa hiari" Asha Baraka.
No comments