Wajane Kutoka Tanzania Bara na Zanzibar Kukutana Katika Kongamano Kubwa Octoba 30 Dar
Taasisi ya Dr. Amon Mkonga Foundation imeandaa kongamano kubwa litakalo wakutanisha wajane jijini Dar es salaam octoba 30 katika ukumbi wa Mlimani City.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya iliyotokewa leo Agosti 13 na mkurugenzi wake Dr. Amon Mkonga imesema kuwa kongamano hilo la siku moja washiriki watatoka Tanzania Bara na Zanzibar.
"Lengo kubwa la kuandaa kongamano hili ni kuwaleta pamoja wajane kubadishana mawazo na uzoefu juu ya changamoto wanazo kabiliana nazo katika maisha yao ya kila siku na kuzipatia ufumbuzi"
Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa washiriki pia watapata fursa ya kupatiwa msaada wa kisheria, Elimu juu ya mila potofu, Bima ya Afya pamoja na elimu ya Uwezeshwaji kiuchumi na mkopo.
Taarifa hiyo ime eleza kuwa watoa mada katika kongamano hilo watakuwa ni wanawake viongozi wastaafu na viongozi maarufu.
Kwa watao taka kushiriki kongamano hili kuwasiliana kupitia namba 0655 638 004 au kupitia barua pepe mkongafoundation@gmail.com
No comments