Mahafali ya 12 Chuo Cha Amana Vijana Centre Yafana Jijini Dar es salam
Wanafunzi wanaohitimu mafunzo ya kozi mbalimbali katika vyuo vya ufundi stadi wameaswa kutumia fursa za mikopo inayotolewa katika halmashauri za wilaya ili waweze kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi nasio kutegemea kuajiriwa pekee.
Akizungumza jijini Dar esalaam Mjumbe wa halmashauri kuu ya Taifa CCM Mkoa wa Dar es salaam, Bw. Yusuph Nasoro wakati wa mahafali ya 12 ya kituo cha Amana Vijana Centre ambapo amewaasa kuacha kutegemea kuajiriwa pekee bali watumie fursa ya mikopo hiyo ili waweze kujiajiri.
"Nimesikia changamoto zenu, mmetaja kwamba eneo lililopo kwa sasa ni finyu, nitakutana na mkuu wa wilaya nimueleze, ndugu zangu kuna wadau wengi tu ambao tukifanya harambee watatusaidia kwahiyo nawaahidi hili nitalifikisha sehemu sahihi na tutapanga lini tufanye hii harambee" alisema Bw. Nasoro
MNEC huyo ambaye alikua mgeni rasmi katika mahafali hayo alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa changamoto zinazokikumba Kituo hicho atatafuta wadau mbalimbali nakufanya harambee ya kuchangia fedha zitakazotumika kuboresha miundombinu ya kituo hicho.
Mkurugenzi mtendeji wa Kituo hicho Philipo Ndokeji alisema kwamba Wanafunzi 16o wamehitimu mafunzo katika fani tofauti zinazotolewa kituoni hapo ikiwemo Udereva, Upambaji, Hotelia, Kompyuta, Ufundi cherehani pamoja Saloon.
Aidha Ndokeji alisema kuwa kituo hicho kitaendelea kutoa elimu bora inayomwezesha kijana kukabiliana na ushindani wa soko la ajira, nakwamba vijana wengi wanaohitimu kituoni hapo wamekua wakifanya vizuri katika taasisi mbalimbali.
Kwa upande wake Katibu wa Taasisi ya Wakati wako ni sasa ambayo inaendeleza vipaji vya kuimba na kucheza kwa vijana nakusaidia watu wenye uhitaji hapa nchini Hassan Ally aliwaasa wahitimu hao kuwa na nidhamu kazini pamoja nakufanya kazi kwa bidii ili waweze kufanikiwa katika kazi zao.
Baadhi ya wahitimu hao akiwemo Jonh Joviti ( Hotelia) na Fatuma ( Kompyuta) walisema kwa nyakati tofauti kuwa watazingatia yale waliyoelekezwa nakwamba elimu waliyoipata itawasaidia kuajiriwa au kujiajiri ili waweze kupata maendeleo yao na kusaidia familia zao.
No comments