MISA TANZANIA Waichamhua Ripoti ya Sheria Ya Takwimu na Sheria ya Huduma ya Mtandao
Wadau kutoka taasisi za kihabari wamepitia na kutoa maoni kwenye ripoti ya Sheria ya Takwimu na Sheria ya huduma za mitandao na posta (Statistics Act, 2010 & EPOCA 2018), kwenye kikao kilichofanyika jijini Dar es Salaaam hivi karibuni.
Kikao hicho kilichoandaliwa na MISA TANZANIA kwa ushrikiano wa IMS (INTERNATIONAL MEDIA SUPPORT) Wadau hao walijadili mambo kadhaa yaliyoainishwa kwenye ripoti ikiwemo maeneo mbalimbali ya sheria hizo mbili ambayo yamekuwa kikwazo na changamato kwa tasnia ya habari.
Baadhi ya maeneo yaliyoguswa na kutolewa maoni na wadau kutoka katika sheria hizo tajwa na kanuni zake ni pamoja na upitiwaji sheria ndogo/kanuni zinazotungwa na TCRA kwani ndizo zinye vipingamizi na ukinzani mkubwa dhidi ya haki ya kutoa na kupokea taarifa.
Pia wadau hao walipendekeza kwamba ripoti hiyo ijumuishe mabadiliko ya mfumo unaozita Redio za kijamii na kuzifanya ziwe kwenye mfumo wa kibiashara litakavyoathiri upatikanaji wa taarifa hasa kwa jamii zilizosahaulika.
Maoni yaliyotolewa na wadau wa habari katika kikao hicho yatatumika kuiboresha ripoti tayari kwa kuombea na kupendekeza mabadiliko ya vipengengele ainishwa, hasa kwa wakati huu ambao wizara husika imeonyesha utayari wa kupokea maoni na mapendekezo ya wadau ili kuiboresha tasnia ya habari nchini.
Akizungumza katika kikao hicho Kaimu Mkurugenzi wa MISA TAN Andrew Marawiti alisema ripoti hiyo imeandaliwa ili kufanyia udukuzi na uzengezi wa mabadiliko ya baadhi ya maeneo ya sheria hizo yanayoonekana kududumiza uhuru wa upatikanaji na utoaji wa habari nchini
No comments