Halmashauri ya Jiji la Ilala Yapata Hati Safi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Amosi Makalla amewataka watendaji wa halamsahauri ya jiji la Dar es alaam pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo kuendelea kusimamia vyema miradi ya maendeleo ili iendane na thamani ya fedha iliyopangwa.
Amesema kuwa Halmashauri ya Manispaa ya ilala ambayo kwa sasa imepanda hadhi nakua halmashuri ya jiji la Ilala imepata hati safi kutokana na taarifa ya mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali (CAG )ambapo hati hiyo imetokana na ushirikiano mzuri kati ya watendaji wa halmashauri hiyo na madiwani.
Akizungumza katika kikao maalumu cha kisheria cha baraza la madiwani kilichokua kinajadili taarifa ya CAG , ambapo kimejadili baadhi ya mapendekezo na hoja zilizotolewa kwenye taarifa hiyo nakuwataka madiwani wawasimamie wataalamu kukamilisha hoja hizo.
"Kupata hati chafu au hati ya mashaka ni jambo la kujitakia, ninae ongea hapa mimi ni mhasibu mkubwa na wakimataifa, ili msipate hati chafu au za mashaka mnatakiwa kuweka ushirikiano , unapoulizwa mbona hiki hakipo toa ushirikiano vinapokosekana baadhi ya vitu kuviambatanisha unapata hati chafu au hati ya mashaka " alisema RC Makala.
Aliwashauri madiwani hao kumtumia vizuri Mkaguzi wa ndani kwani yeye ndo atakae washauri mahali wanapokosea nakwamba wasimuone adui bali anawatakia mema kwenye utekelezaji wa kazi zao.
Pia ameisisitiza halmashauri hiyo kufuatilia madeni ya takribani bilioni 11 wanayodai kutoka kwa wadau mbalimbali , lakini pia ameshauri kulipa madeni ambayo halmashauri ya jiji hilo inadaiwa na wadau mbalimbali ili kuepuka kupelekwa mahakamani nakupata hati chafu.
"Hongereni sana Kupata hati safi miaka mitano mfululizo hatua hii inawafanya mjenge imani kwa wananchi ambao ndo wachangiaji wa fedha hizi za maendeleo pamoja na mashirika mbalimbali ya maendeleo kuamini kwamba fedha wanazowekeza zinakua salama na zinatekeleza yale yaliokusudiwa " alisema RC Makalla. .
Awali Meya wa Jiji la Dar es salaam Omary Kumbilamoto amesema kuwa kuwepo kwa mafunzo mbalimbali kwa madiwani pamoja na ushirikiano kati ya watendaji na madiwani umechangia kwa kiasi kikubwa kupata hati safi mfululizo.
Taarifa hiyo ya CAG imesomwa mbele ya baraza la madiwani na Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Ilala Jumanne Shauri nakujadiliwa na madiwani wa halmashauri ya jiji la Ilala.
No comments