Shonza Azindua Tamasha la Kutoa Elimu kwa wadau wa Filamu Kupitia Mtandao "HATUA" Jijini Dar
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Juliana Shonza, leo tarehe 02 Julai, 2020 akiambatana na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Ndg. Godfrey Mngereza na Kaimu Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt. Kiagho Kilonzo.
Mhe Shonza alizindua Tamasha hilo ambalo ni mahususi kwa ajili ya kutoa elimu kwa wadau wa Filamu ya namna bora ya kuuza na kusambaza kazi za Filamu kupitia teknolojia ya mtandao liitwalo "HATUA".
Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na msanii GABO kwa kushirikiana Swahiliflix limefanyika katika viwanja vya Mbagala Zakiem, Jijini Dar es salaam.
No comments