Breaking News

Rais MAGUFULI Ashisha Neema Jimbo La UKONGA, Rc MAKONDA Athibitisha Kupokea Fedha za Ujenzi wa KM 29 za Barabara Mpya za Lami.


Kufuatia kilio cha Muda mrefu cha Wananchi wa Jimbo la Ukonga na juu ya Ubovu wa Barabara, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amesema Rais Dkt. John Magufuli ameridhia kutoa fedha za Ujenzi wa Barabara Mpya jimboni humo kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Km 29 Chini ya Mradi wa DMDP kwa fedha kutoka Bank ya Dunia.

Akizungumza katika simu ya 5 wa Mwendelezo wa Ziara ya siku 10 jijini Dar es salaam ya kukabidhi Miradi kwa Chama cha Mapinduzi CCM Jimbo la Ukonga ambapo ameeleza miongoni mwa Barabara hizo ni Km 12 za kutoka Kwa Mpalange kwenda Kilungule, Mwanagati, Kitunda na kuishia Banana.

Alisema barabara nyingine zinazojengwa ni Km 16.6 kuanzia Pungu Majoe kupitia kwa Mngondole, Kivule hospital na kuishia Kitunda pamoja na km 5 inayoanzia Chanika kupitia Msumbiji kuelekea Homboza.

Aidha RC Makonda amemuelekeza Mkandarasi wa mradi usambazaji umeme wa REA kata 8 na mitaa 25 ya Zingiziwa kuhakikisha ifikapo Agost 31mitaa yote iwe imeunganishwa na umeme kwa gharama ya Tsh 27,000 na sio 320,000 iliyopangwa na TANESCO.

Katika ziara hiyo RC Makonda amekabidhi kwa Chama cha mapinduzi miradi mbalimbali ikiwemo Machinjio ya Vingunguti, Hospital ya Wilaya ya Kivule A na B, Mitambo ya Umeme Kinyerezi one na Two, Mtambo wa Gas wa TPDC na Mradi wa kusambaza umeme Zingiziwa.

Miradi mingine ni Ujenzi wa Soko la Kisutu, Jengo la Abiria la Terminal Three, Ujenzi wa Daraja la Ulongoni B, Ujenzi wa Barabara ya kuanzia Banana, Kitunda na Kivule zenye urefu wa Km 3.2.

No comments