Rc Makonda Akabidhi CCM Miradi Iliyotekelezwa na Seriikali ya Awamu ya Tano Jimbo ka Kawe
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo ameendelea na ziara yake ya kukabidhi miradi Mbalimbali iliyotekelezwa na serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli kwa Chama cha Mapinduzi CCM na kuwahimiza Wananchi kuchagua Viongozi wanaoweza kutatua kero zao.
Miongoni mwa Miradi aliyoikabidhi RC Makonda iliyotekelezwa kupitia Ilani ya CCM kwa upande wa Jimbo la Kinondoni ni Mradi wa Soko la Magomeni lenye thamani ya Shilingi Bilioni 8.9, Ujenzi wa Jengo la Mama na Mtoto hospital ya Mwananyamala inayogharimu Bilioni 3 na Mradi wa Ujenzi wa Kiwanja Cha Mpira Mwenge chenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.5.
Aidha RC Makonda pia amekabidhi Mradi wa Ujenzi Barabara ya Morocco hadi mwenge yenye thamani ya Bilioni 69.7, Mradi wa Kituo cha Mabasi Mwenge Bilioni 2.5 na Kituo cha Afya Kigogo chenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.5.
Kesho Jumatano RC Makonda ataendelea na ziara yake kwenye Jimbo la Kibamba ambapo atakabidhi miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Chama cha Mapinduzi CCM.
No comments