Rc MAKONDA Awaagiza TAKUKURU Kufanyika Uchunguzi wa Bilioni 33 Fedha za Mikopo ya 10% za Manispaa kuona Iliwafika Walengwa
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda amewataka Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa TAKUKURU kuanza Mara moja uchunguzi Fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 33 za mikopo ya 10% iliyotengwa kwaajili ya makundi ya Vijana, Kinamama na Walemavu katika Halmashauri kama fedha hizo zinawafikia kwa walengwa.
RC Makonda ametoa agizo hilo wakati wa Mwendelezo wa Ziara ya Kukabidhi Miradi kwa Chama cha Mapinduzi Jimbo la Ubungo na kuwaelekeza kuhakikisha kabla ya Julai 20 anapatiwa mchanganua wa namna pesa hiyo imetumika kwakuwa Rais Magufuli aliondoa Riba kwenye mkopo huo ili kuyawezesha kiuchumi makundi hayo.
Miongoni mwa Miradi aliyokabidhi ni Daraja la Juu Ubungo lenye thamani ya Bilioni 299, Upanuzi wa Mto Ng'ombe Bilioni 32.5, Ujenzi wa Barabara ya Shekilango na Viunga vyake Bilioni 26 na Ujenzi Wa jengo la Wodi ya Wagonjwa na Upasuaji Hospital ya Palestina.
Miradi mingine aliyokabidhi RC Makonda ni Ujenzi miundombinu ya Madarasa 8, Matundu 12 ya Vyoo na uzio kwenye Shule ya Ubungo plaza* pamoja na kukagua Vikundi 20 vya wajasiriamali waliokopeshwa fedha kupitia 10% za Manispaa.
Ziara hiyo itaendelea tena siku ya kesho kwa majimbo ya Ilala, Segerea na Ukonga ambapo atakabidhi miradi mbalimbali ya Maendeleo.
No comments