Neema kwa Wajasiliamali Wadogo Nchini Mwekezaji Atangaza Kutoa Mikopo Isiyo na Riba.. Nyumba, Viwanja na Magari
Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) Bw. Ussi Said Suleman akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Wafanyabiashara wadogo wametakiwa kuchangamkia fursa ya kujiunga na kuwekeza katika Kampuni ya Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) ambayo inatoa mikopo ya aina mbalimbali isiyo na riba pamoja kutoa faida kila mwezi.
Kampuni ya Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) imelenga kuwasaidia na kukuza mitaji ya wafanyabiashara wadogo, kutoa mafunzo ya ujasiriamali ili kuhakikisha wanapiga hatua katika nyanja za kiuchumi.
Akizungumza na waandishi wa habari wiki hii jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) Bw. Ussi Said Suleman, amesema kuwa lengo ni kuunga mkono Serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar katika kuhakikisha wafanyabiashara wadogo wanafanikiwa.
Bw. Suleman amesema kuwa baada ya mfanyabiashara mdogo kujiunga na kuwekeza kuanzia sh. 50,000 atapata fursa ya kukopeshwa kulingana na uwitaji wake ikiwemo mtaji, kiwanja, nyumba, bajaji, friji, magari ili kuhakikisha anapiga hatua kimaendeleo.
“Mtu yoyote anaweza kujiunga na Kampuni yetu kwa kufika ofisini kwetu Zanzibar au kujiunga kwa kutembelea mtandao wetu wa Online Small Capital Mobile au kupiga simu ya kiganjani kupita namba 0718 12 55 77, 0776 423 639”amesema Bw. Suleman.
Bw. Suleman amefafanua kuwa ili mtu aweze kujiunga anatakiwa kuchukua fomu kwa gharama ndogo ya sh.10, 000 ambayo itamuwezesha kujiunga na kuanza mpango wa kufikia ndoto zake kibiashara.
“Ni fursa kubwa kwa watu wenye kipato cha chini, lengo letu ni kuwasaidia ili kutimiza ndoto zao, tunafanya hivyo kutokana tunajua wengi hawana mitaji ya kuanzisha biashara, lakini wakijunga na kampuni wanapata uwezo kukopa na kupiga hatua za kiuchumi” amesema Bw. Suleman.
Ameeleza kuwa mpaka sasa watu 1,500 wamechangamkia fursa kwa kujiunga na Kampuni ya Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC), huku 500 wemeshapatiwa mikopo ambayo ina mifumo rafiki ya kuwalipia madeni kupitia faida yao ya kila mwezi.
Amesema lengo ni kuwafikia wanachama zaidi ya 5,000 wenye kipato cha chini ili waweze kuwasaidia kupitia ubunifu wa kuwekeza kupitia simu ya kiganjani.
Bw. Suleman ametoa wito kwa serikali ya Tanzania Bara na Zanzibar kuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku kwa makampuni yanayofanya vizuri ili ziendelee kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali katika jamii.
Kampuni ya Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) imeanzishwa mwaka 2019 Zanzibar ambayo imelenga zaidi kuwasaidia wafanyabiashara wadogo ili waweze kupiga hatua kiuchumi kwa kuwakopesha mikopo isiyo na riba baada ya kujiunga.
Kampuni ya Uwekezaji ya Online Small Capital Mobile (OSC) inatoa mikopo ya mbalimbali ikiwemo magari na nyumba pamoja kutoa ushauri wa kibiashara.
Mashaallah mashaallah good
ReplyDelete