Breaking News

CUF Yapuliza Rasmi kipenga rasmi kuelekea Uchaguzi Mkuu


Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi CUF Taifa, bw Juma Khalaga, wakati wa uzinduzi wa mchakato wa uchaguzi wa CUF kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Chama cha Wananchi (CUF) kimepuliza kipenga cha uchaguzi ndani ya chama na kutoa ratiba kamili ya kura za maoni ambapo kimesema mgombea atakayetoa rushwa akibainika Baraza Kuu litamuondosha katika kinyanganyiro.

Pia kimekaribisha chama chochote chenye dhamira ya dhati kitakachotaka washirikiane kuelekea Uchaguzi Mkuu mwaka huu
.
Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi CUF Taifa, Juma Khalagai ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa mchakato wa uchaguzi wa CUF kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020.

Alisema wanachama wote wenye sifa wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za kukiwakilisha chama katika Uchaguzi Mkuu 2020 ambapo wamewahakikshia kuwa chama hakina wagombea wateule.

”Ratiba yetu imeanza leo kwa zoezi la kuandaa fomu za wagombea na inatarajiwa kuhitimishwa tarehe 27,7, 2020 ambapo wagombea urais wa tiketi ya CUF wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar watateuliwaa,”alisisitiza.

Ameongeza kuwa, katikati ya tarehe hizo kutakuwepo na matukio mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuandaa kura za maoni katika ngazi za kata na wilaya kwa Tanzania Bara na jimbo kwa Zanzibar.

Alisema, wanatarajia kuweka wagombea udiwani, uwakilishi wa ubunge, lakini pia watasimamisha wagombea urais wawili mmoja akisimama kwa ajili ya urais Zanzibar na mwingine atasimama kwa ajili ya urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments