Mchungaji Mwakitalu na Rose Mgeta Wasimikwa Rasmi Kanisa la Mlima wa Moto
Kanisa la mlima wa moto la MIKOCHENI Jijini Dar es salaam limefanya ibada maalum kuwasimika maskofu wa mda wa kanisa hilo kufatia ya kifo Cha aliyekuwa askofu wa kanisa hilo mchungaji Dkt. GETRUDE RWAKATARE.
Wakizungumza na mamia ya waumini walioudhulia ibada hiyo mara baada ya kusimikwa rasmi mchungaji Wiliaum Mwakitalu na Mchungaji Rose Mgeta wameahidi kuwatumikia kwa dhati ikiwemo umoja na mshikamano
"Ndugu zangu jukumu mlilotupatia ni zito tutalitekeleza kwa dhati na kuhakikisha tunawatumikia sambamba na kuhakikisha umoja na mshikamano ubakuwepo kati yetu" Alisema.
Alisema katika kipindi cha uongozi wa watajitahidi kuakikisha wanatekeleza wajibu wao kwa weledi zaidi kwa lengo ya kuhakikisha kanisa linasimama kufukia malengo yake
Mchungaji Wiliaum Mwakitalu akifanyiwa maombi kusimikwa rasmi kuwa mchungaji wa Kanisa la mlima wa moto katika ibada iliyofanyika kanisani hapo jijini Dar es salaam.
Mchungaji Rose Mgeta akifanyiwa maombi kusimikwa rasmi kuwa mchungaji wa Kanisa la mlima wa moto katika ibada iliyofanyika kanisani hapo jijini Dar es salaam
No comments