Felix Mkosamali ahama NCCR-Mageuzi ajiunga Chadema
Aliyewahi kuwa MBUNGE wa Jimbo la Muhambwe Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma, Felix Mkosamali, ametangaza kukihama chama cha NCCR-Mageuzi na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
Mkosamali mbali na kuhamia CHADEMA pia ametangaza nia ya kugombea tena
Jimbo la Muhambwe na kusisitiza kuwa atapambana kuhakikisha anawatumikia tena wananchi kwa mara nyingine.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Mkosamali amesema ameamua kujiunga na CHADEMA kwa kuwa ni chama chenye kusimamia haki.
“Nimeamua kujiunga na CHADEMA ni chama chenye msimamo wa nguvu katika
kutetea maslahi ya Watanzania na nchi kwa ujumla,”amesema Mkosamali
Amesema CHADEMA ni chama ambacho kinawatumikia wananchi kwa moyo mmoja tofauti na vyama vingine.Ameongeza kuwa NCCR-Mageuzi kwa sasa imekuwa chama kisichoeleweka katika misimamo yake .
“NCCR-Mageuzi kimekuwa kama mdudu kinyonga mara wa bluu au kijani…
hata kauli za viongozi wao wa kitaifa zinaonesha kuwa hawako tayari
kupambania majimbo, wanasubiri kupewa dola, amesema Mkosamali
Aidha amesema atahakikisha anawashawishi wananchi kudai Katiba, kwani
bila kufanya hivyo itakuwa ni ngumu kuiondoa CCM madarakani.
No comments