Waziri MAKAMBA Awataka Watendaji Wa NEMC Kutekeleza Majukumu Yao Kwa Weledi Katika Zoezi La Kufatiaji Mifuko Ya Plastiki
WAZIRI wa nchi ofisi ya makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, mhe. January Makamba, amewaagiza watendaji wa Baraza la Taifa la hifadhi na usimamizi wa mazingira (NEMC) kuhakikisha wanafanya kazi ya msako ya mifuko ya plastiki mpaka siku za mapumziko ili kuondokana na mifuko hiyo.
Akizungumza katika ziara ya kufanya ukaguzi katika soko la kariakoo kuangalia utekelezaji wa agizo la kuanzia leo tarehe moja mwezi wa sita la kutotumia mifuko ya plasticki kwa lengo la kulinda mazingira.
Amesema katika utekelezaji wa agizo hilo ni wakati wa bodi ya NEMC kuhakikisha wafanya kazi ambao wapo kwenye kikosi kazi cha kukagua watumiaji wa mifuko hiyo iliyokatazwa kufanya kazi kwa kasi zaidi ikiwemo kufanya kazi mpaka siku za mapumziko.
"Katika kipindi hiki cha utekelezaji wa sheria hii mpya ni wakati wa bodi ya Nemc kuwataka wafanya kazi waliopewa kufanya kazi ya ukaguzi wa mifuko kufanya kazi mpaka siku ya mapumziko kuhakikisha mifuko hii inapotea."amesema Makamba.
Makamba amesema nchi haijakurupuka
Kaukataza matumizi ya mifuko ya plastiki baada ya kubaini mifuko hiyo ibaharibu mazingira ambapo akitoa mfano endapo Tanzania ikiendelea na matumizi ya mifuko hiyo katika kipindi cha miaka 20 ijayo Baharini kutakuwa na mifuko mingi kuzidi samaki jambo analodai ni hatari kwa mazingira.
Hata hivyo, Waziri Makamba amesema shehena ya mifuko ya plastiki iliyopatikana kutoka kwa watumiaji itapelekwa kutengenezea Bomba na madawati hivyo akiwasihi wananchi kusalimisha ya plastiski kwenye mamlaka husika
Kwa upande wake mwenyekiti wa Bodi ya ya NEMC,Profesa Esnati Osinde amesema watataendelea kutoa elimu hadi kwa viongozi wa dini kuhakikisha wananchi wanapata elimu juu ya madhara ya matumizi ya mifuko ya plastiki.
Mbona vibebeo vyeupe vile, bado vinatumika na ukitaka ukweli nitafute 0656670545.
ReplyDelete