Breaking News

TIC Yatoa Ufafanuzi Tuhuma Alizotoa Mhe ZITTO Kabwe

Kituo cha uwekezaji Tanzania (TIC), kimetoa ufafanuzi juu ya tuhuma zilizotolewa na mbunge wa kigoma mjini mhe. Zotto kwabwe  kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kuhusu hali ya uwekezaji nchini.

Akizungumza jijini Dar es salaam, mkurugenzi wa TIC Bw, Geoffrey Mwambe alisema tuhuma hizo hazina ukweli wowote bali miradi yote ambayo anadai kuwa imesimama ni kutokana na kuendelea kwa mazungumzo kati ya serikali na wawekezaji.

“Mfano mradi wa liganga na Mchuchuma ni moja ya mradi mkubwa wa uwekezaji amabo unahusisha kuchimba na kufua umeme unaotokana na makaa ya mawe ambao unatekelezwa kupitia kampuni ya Tanzania China International Mineral Resources Ltd kwa ubia na serikali kupitia shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) kwa asilimia 20 na kampuni ya Sichuan Hongda ya china yenye asilimia 80 ambapo mpaka kukamilika kwake utazalisha umeme 600 MW” alisema Bw. Mwambe.

Akielezea mradi wa usindikaji gesi wa NLG ambao upo katika mchakato wa majadiliano baina ya wawekezaji na shirika la Taifa la Maendeleo ya Petrol  (TPDC) ambao unataji kujengwa mkoani Lindi alisema wawekezaji wa mradi huo ni kampuni ya Equinor yenye asilimia 65 na Exxor Mobil mwenye asilimia 25.

“Miradi yote ambayo amehitaja mhe. Zitto Kabwe ipo katika awamu mbalimbali ya utekelezwaji nitoe rai kwa mhe Kabwe aache kupotosha juu ya miradi hiyo na kama akihitaji taarifa za kuhusu mwenendo wa miradi hiyo anaweza kupatiwa kuliko kupotoshaji anaofanya” alisema bw. Mwambe  

No comments