Breaking News

Wakili Manyama: Rais Ndio Kioo Cha Nchi.. Kumchafua Rais Ni Kuichafua Nchi.

Wakili wa Kujitegemea Bw. Leornard Manyama ameelezea kusikitishwa na kauli za baadhi ya wasomi na wawakilishi kuunga mkono kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na Mhe Tundu Lisu kuwa matamshi anayoyatoa ayajalenga kuichafua taifa badala yake yamekuwa yakilenga serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Wakili Manyama alisema amesikitishwa kitendo cha baadhi ya wasomi na wawakilishi hao kwa kuungana na mbunge huyo kupotosha pamoja na kufahamu kuwa popote Duniani Rais ndio Taswira ya nchi ivyo kitendo cha Kumchafua Rais ni sawa na kuichafua nchi.

"Nimewaiteni hapa kutoa ufafanuzi kufatia kuwepo na upotoshaji kubwa ambao umekuwa ukifanyika kupitia mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kuwa matamshi ambayo yanatolewa na mhe Tundu Lisu si kwa lengo la kuichafua nchi bali yamelenga serikali ambayo inaongozwa na Mhe Rais Magufuli wakijua kabisa uwezi kutenganisha nchi na serikali" Alisema Wakili Manyama.

Alisema serikali uchaguliwa na wananchi kwa mujibu wa katiba hivyo Rais ni kioo cha nchi na kama rais atachafuliwa wananchi ambao wamechangua na kumweka madarakani wote watakuwa wamechaguliwa hivyo kitendo kinachofanywa na mhe Lisu ni cha kukemewa  kwan kina mahala makubwa kwa taifa. 

Aidha wakili Manyama Ameyataja madhala ambayo yanaweza kulipata taifa endapo kama watanzania awataungana kumkemea kauli za kusaliti ambazo zimekuwa zikitolewa na mhe Lisu kuwa ni sawa na yaliyotokea nchini Libya ivyo kuwataka watanzania kujitokeza bila kujali itikadi zao kumpinga.

"Kwa anachokifanya Mhe Lisu ni kusaliti nchi atakiwi kuungwa mkono badala yake kama taifa ipo haja ya kuungana kukemea tabia hiyo kwani ina mahala makubwa sana kwa taifa" Alisema.

No comments