Tanzania Kujengwa kiwanda cha Kisasa Cha Vifaa Vya Magari Na Vifaa Vya Elektroniki
Akizungumza jijini Dar es Salaam katika kikao cha pamoja kati ya wawekezaji na watendaji kutoka taasisi mbalimbali Waziri Kairuki amesema kuwa wawekezaji hao wako tayari kuwekeza kwenye maeneo mbalimbali nchini.
"Hii ni fursa kwetu kutokana na wawekezaji kuwa tayali kuwekeza katika sekta mbalimbali ikiwemo vifaa vya majumbani, pamoja na vifaa vya magari, ujenzi na mashine za mawasiliano na usalama vitakavyouzwa soko la ndani na nje ya nchini" Alisema Mhe Kairuki.
Alisema kupitia uwekezaji huo kwa kushirikiana na serikali utawezesha kujengwa karakana ya kurepea magari itakayowezesha vijana waliosomea fani mbalimbali katika vyuo vya ufundi stadi kuweza kupata sehemu ya kufanyia mafunzo kwa vitendo pamoja na kupata ajira na utaalamu wa kiwango cha juu zaidi.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Uwekezaji TIC John Mnali alisema kampuni hiyo tayari imewekeza katika nchi nyingi Afrika na endapo watafungua Kiwanda hapa Tanzania itapewa ushirikiano wa kutosha ili kuiwezesha kuvutiwa kuwekeza zaidi nchini.
"kampuni hii tayari imewekeza katika nchi nyingi Afrika na endapo watafungua Kiwanda hapa Tanzania wataweza kuzalisha vifaa mbalimbali kwa matumizi ya nyumbani na viwandani" Alisema bw Mnali.
No comments