Breaking News

MUSIBA: Anachofanya Mhe Lissu Ni Usaliti Kwa Taifa... Namfungulia kesi Ya Uhaini

Mwanaharakati huru na mkurugenzi wa CZI bw, Cyprian Musiba, amesema anatarajia kumfungulia kesi ya uhaini Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu kufatia matamshi ambayo amekuwa aliyatoa akiwa katika ziara ya nchi mbalimbali kwa taifa. 

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Musiba alisema anachukua hatua hiyo kwa kile alichodai kuwa Lissu ni msaliti kwani anatoa siri za nchi nje.

“Namshitaki kwa kutoa siri za nchi nje, nampeleka mahakamani haiwezekani ahubiri kutaka kumpindua rais,” alisema Musiba.

Musiba alieleza kuwa mbunge huyo amekuwa akifanya upotoshaji kwa lengo la kumchafua Rais na Serikali ambapo alitoa mfano kuwa Lissu katika moja ya mikutano yake huko nje alisema kuwa vyombo vya usalama nchini vimeua watu 400.

Aliongeza kuwa katika vikao vyake vya siri baada ya vile vya wazi amekuwa akitaka rais atolewe madarakani lakini pia akishinikiza Tanzania kunyimwa misaada kwa kile anachodai kuwa kunauminywaji wa demokrasia.

Alimtaka Mwanasheria huyo mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuacha kuichafua nchi na badala yake kama anaona Katiba inavunjwa afuate taratibu na kufungua kesi ya Kikatiba.

Akizungumza kuhusu kupigwa risasi kwa Lissu Musiba alidai kuwa tukio hilo lilikuwa ni mpango wa viongozi wa Chadema ili kutimiza adhima ya mbunge huyo kuogombea urais mwaka 2020 na kwamba hakupigwa na risasi halisi.

Aliwataka wananchi kuendela kulinda na kutunza amani iliyopo na kutoa rai kwao kupuuza madai ya Lissu kwani lengo lake ni kuivuruga nchi.

No comments