Breaking News

TGNP Mtandao Kuzindua Kampeni Kubwa Ya Ulinzi Wa Mtoto Jijini Dar

TGNP mtandao wameamdaa kampeni kubwa ya ulinzi wa mtoto itakayoitwa 1-5-5 "Namlinda" itakayofanyika tarehe 27 mwezi huu kuunga mkono jitihada za serikali kutokomoeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwa asilimia 50 ifikipo 2020.

Akizungumza jijini Dar es salaam Mfuatiliaji na Mwibuaji matukio dhidi ya ukatili wa wanawake na watoto wa TGNP Mtandao Bi. Janeth Mawinza alisema kampeni hiyo imelenga kutoa elimu kwa jamii juu ya athari za ukatili wa kingono kwa watoto na umuhimu wa kuwalinda dhidi  ya vitendo hivyo itazinduliwa na IGP wa jeshi la polisi Saimoni Sirro

"Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa mwaka juni 2018 inaonyesha kuwa matukio ya ukatili wa kingono miongoni mwa watoto yameongezeka ambapo jumla ya watoto 394 ubakwa kila mwezi nchini, huku matukio ya kulawiti nayo yakiongezeka kutoka 12 mwez Januari mpaka juni 2017 hadi matukio 533 Juni 2018" Alisema Bi. Mawinza. 

Alisema kwa mujibu wa ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa kila msichana mmoja kati ya watatu na kila wavulana mmoja kati ya saba tayali wameshakutana na ukatili wa kingono kabla ya kufikia miaka 18 katika mikoa ya Iringa na Dar es Salaam
Mapema Mratibu wa kampeni hiyo Bi. Anna Sangai alisema kampeni inalenga kujemga nguvu za pamoja na wadau mbalimbali kuweka mikakati ya pamoja ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono hili kuakikisha kila mtu katika jamii anawajibika kumlinda mtoto. 

"Sambamba na kuunga mkono jitihada za serikali juu ya kutokomeza ukatili wa kingono kwa watoto nchini, kampeni hii pia itatoa elimu kwa jamii juu ya athari za ukatili wa kingono kwa watoto na umuhimu wa kuwalinda na ukatili huo sambamba na kutathimini na kuibua mijadala katika jamii, kuamasisha jamii kuzuia vitendo hivi na kutoa taarifa ili wahusika wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria" Alisema Bi. Sangai.

No comments