DCP Nziku: Azindua Kampeni Ya "1-5-5 Nitamlinda" Awataka Wazazi Na Walezi kushiriki Kikamilifu Vita Dhidi Ya Ukatili Wa Kijinsia Kwa Watoto.
Dar es salaam :
Jamii imetakiwa kuwa karibu na watoto hususani wa kike ili kuwalinda dhidi ya vitendo vya ukatili wa kingono.
Akizungumwa jiji dar es salam katika uzinduzi wa kampeni ya ulinzi wa mtoto dhidi ya ukatili wa kingono iliyoandaliw na TGNP mtandao ya "1-5-5 Namlinda" Mkuu wa dawati la Jinsia Naibu kamishna wa police Mary Nziku alisema wazazi na walezi ndo wenye jukumu la kwanza la kumlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili.
"katika vita hii ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsi kwa watoto linaanzia kwa mzazi na walezi kwani wao ndio wenye jukumu la kwanza kuhakikisha wanamlinda mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa watoto" alisema Dcp Nziku.
Alisema pamoja na kuhamasisha wazazi na walezi kushiriki kikamilifu pia serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali imekuwa ikitoa elimu kwa jamii juu ya hatua zinazotakiwa kuchukuliwa pindi itakapobainika uwepo wa vitendo ivyo katika maeneo yao kwa lengo la kuhakikisha wanavitokomeza kabisa vitendo ivyo katika jamii.
Dcp Nziku aliongeza kuwa pamoja najihada zote ambazo serikali imekuwa ikizichukua kutokomeza vitendo ivyo bado takwimu zilizopo zinaonyesha kuwa tatizo la ukatili hususani wa kingono kwa watoto bado ni changamoto kubwa nchini.
"kwa mujibu wa Tafiti vitendo ivyo vikifanywa na watu wa karibu ivyo kupitia kampeni hii ya "1-5-5 Namlinda" nategemea itatoa matokeo chanya hususani kuongeza uelewa kwa wazazi na walezi hivyo nyumbani kuwa ni sehemu salama kwa watoto.
"Kwa mujibu wa takwimu matukio ya unyanyasaji wa kingono kwa watoto nchini zinaonyesha kuwa kila mtoto moja kati ya watatu wenye umri wa chini ya 18 tayali ameshakutana na tatizo hili, muhimu kila mtu katika jamii kwa nafasi yake kutimiza wajibu wake kumfanya mtoto afurahie utoto wake, ujana wake na uzee wake" Alisema bi. Liundi.
No comments