Breaking News

Prof Lipumba Ateuwa Majina 9 Ya Wajumbe Wapya Wa Bodi Ya Wadhamini CUF

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba akiongea katika mkutano na waandishi wa habari mapema leo tarehe 21 Februari uliofanyika makao makuu ya chama hicho buguruni jijini Dar es Salaam. 

Dar es Salaam.
Baraza Kuu Taifa Chama cha Wananchi (CUF) kimeteuwa wajumbe wapya tisa wa bodi ya wadhamini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo  jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF) Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kuwa kupitia kikao cha baraza Kuu la Uongozi Taifa kilichokaa Februari I9 mwaka huu wameweza kuteuwa majina 9 ya wajumbe wa bodi.

Amewataka walioteuliwa na baraza kuu kutoka Tanzania bara ni Peter Malebo, Abdul Magomba, Hajira Silia, Amina Mshamu pamoja na Aziz Daghesh. Kwa Upande wa Zanzibar ni Salha Mohamed, Asha Suleiman, Suleiman Issa na Mussa Kombo.

Alisema mara ya kukamilisha uteuzi huo, Kaimu Katibu wa CUF tayari amewasilisha barua ya maombi ya kusajili Bodi ya Wadhamini kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili na Udhamini(RITA), huku akiambatanisha na fomu husika ya kumbukumbu za kikao cha baraza kuu kilichofanya uteuzi.

"Mara baada ya kukamilisha uteuzi huo, Kaimu Katibu wa CUF tayari amewasilisha barua ya maombi ya kusajili Bodi ya Wadhamini kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili na Udhamini(RITA),Nakala ya barua na kumbukumbu za kikao zimewasilisha kwa msajili wa vyama vya siasa" Alisema Profesa Lipumba.

Katika hatua nyengine amefafanua kuwa baraza kuu limeridhia na utendaji wa bodi iliyoteuliwa machi 20I7 na kushauri majina wa wajumbe hao yapendekezwe.

Hata hivyo hivi karibuni Mahakama Kuu nchini Tanzania imetoa uamuzi wa kesi kuhusu mvutano wa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Chama Cha Wananchi (CUF), ikiwakataa wajumbe wapya waliokuwa wameteuliwa na timu Lipumba [Profesa Ibrahim] na timu Seif [Maalim Sharif Hamad].

Kupitia hukumu yake iliyosomwa jijini Dar es Salaam, Mahakama Kuu imeeleza kuwa wajumbe wa pande zote mbili hawakukidhi vigezo vya kuwa wajumbe wa Bodi ya Wadhamini, hivyo uteuzi wao umetenguliwa.

No comments