ULIMWENGU: Wananchi, Viongozi Jikiteni Katika Kutenda Haki Kwa Wengine
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgjxReWY5A98fH6MAdQc4U2q3lud-T8njD_TOBVArENxtAlABq9JgJhb-MEwvJxCWY7xIuuF3A7ock6HotLmohWPI9liv3DiogwgJWtuS8TVmj9Oqp4A_8fXCyo8iQOtuYimnOMe7cb067u/s640/IMG_20190220_181303.jpg)
Mwandishi Nguli nchini Jenerali Ulimwengu, akiwasilisha mada katika kongamano la Haki na Wajibu wa Raia lililoandaliwa na jukwaa la Change Tanzania jijini Dar es Salaam.
Dar es Salaam
Jamii imetakiwa kujikita katika kuhakikisha inasimamia haki na usawa pamoja na utawala wa kisheria kwani ndio msingi wa maendeleo na usawa katika taifa lolote duniani.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati akiwasilisha mada katika kongamano la haki na wajibu wa raia, Mwandishi Mkongwe nchini Jenerali Ulimwengu, alisema ipo aja kama taifa kujikita zaidi katika kutenda haki kuanzia katika ngazi ya familia na katika mihimili yote ya uongozi nchini.
“Kama Taifa Tunatakiwa kutenda haki kwa kila mtu na kuachana na tabia hasa viongozi kufanya mambo ya uvunjifu wa haki kwa kutumia kigezo cha kutekeleza maagizo kutoka juu bila kujali athari zake,” alisema Ulimwengu.
Alisema kumekuwepo na changamano kubwa kwa wananchi wengi kutokuelewa haki zao za msingi kikatiba jambo ambalo limekuwa likipelekea wengi wao kushindwa kutambua wajibu wao na haki zao kwa mujibu wa katiba..
"Nitoe rai hasa kwa viongozi na vijana kujitolea kutetea watu wasiowajua, wanyonge, kuwa waaminifu zaidi ya kuwa watiifu, kushiriki katika maendeleo ya nchi, kukemea maovu na kutenda mema" Alisema Bw. Ulimwengu.
Katika hatua nyingine Bw. Ulimwengu amewataka wanaharakati wanaoendelsha shughuli zao kutokuogopa kufa kwa sababu ya kutetea haki kwani kuogopa hilo ni ujinga.
“Kila mtu atakufa bila kujali sababu, kufa ni suala la muda tu na kuogopa kufa ni ujinga, bora kufa kwa kutetea jambo la maana kuliko kufa kwa mambo ya upuuzi, alisema Ulimwengu.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgzy-vDCXTAJRnHg-k1GDwj-v1ix6fv8gPGvEzexgz4WbS0mYK6-zxhJkbQXFoToFqLQXuiI3Z5OfAl34GnSdvxheSSVQBUWeVeuk2zyCBYP-fKEHocLwPPwgsZ0x3dQf9kiyqSeRZs_uez/s640/IMG_20190220_181002.jpg)
Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Change Tanzani Maria Sarungi, akifafanua jambo katika kongamano la Haki na Wajibu wa Raia jijini Dar es Salaam.
Mapema akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa jukwaa la change Tanzania Bi, Maria Sarungi alisema jukwaa hilo ambalo lilianzishwa mwaka 2012, malengo yake ni kuelimisha na na kusaidia wanachama wake watakaoathirika na sheria ya makosa ya mitandaoni.
Alisema lengo la kongamano hilo ni kukumbusha wanachama wajibu wao wa msingi na kuimarisha mtandao wa uanaharakati katika mabadiliko chanya na kuunganisha vijana kutafakari na kujenga maarifa juu ya haki na wajibu wao kwa Taifa katika maamuzi badala ya kuwaachia wanasiasa.
Naye Mratibu wa Taifa wa Change Tanzania Mshabaha Mashabaha alisema hilo ni jukwa la pili kuanzishwa na asasi hiyo tangu 2016.
“Change Tanzania ni harakati zinazosukuma na kuhamasisha maendeleo kwa kutumia mitandao ya kijamii, kusimamia uhuru wa kujieleza wa wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa fursa kwa wananchi kujadili, kukosoa na kutoa taarifa kupitia mitandao,” alifafanua Mshabaha.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Taasisi ya Twaweza bi, Annastazia Rugaba alisema nafalijika kuona vijana wengi wamejitokeza kushiriki katika kongamano hilo na kuchangia mambo mbalombali yalio na lengo la kuleta matokeo chanya kwa taofa.
"Nimevutiwa sana na michango ya Vijana walio changia katika jukwaa hili kwa kuona vijana wakijengewa uwezo na fikra mpya za kutambua wajibu wao kwa Taifa badala ya kuwa walalamikaji tu mitandaoni wakidai haki zao au kukosoa uwajibikaji wa viongozi" Alisema bi. Ruaba
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjAoxS5J-7pkiGQBRqncUyNd4RpbwmCaxeETAdgfvBd3AiaMMw-Bm5610V6exYErkMJr-DRvq7BjYkuJcTQnVIWJM1bvGZZUJFJpeByEUPZhf57NTIfaInD-H_CotVBLRfJ57HpUwuohPJx/s640/IMG_20190220_181232.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg8gfsBj4SsBP4yU9RpHDsktWy5TXcSZjzkeGGMSRQwIZXfX4Q78QkGv6oCbPfPgCYsFxtWeDiPP5qzW30wQDnSUVxya_pwPDd_r3td3uKvOge0C4m5c3OY60zi7Pdkion8soGkKEmlYQ_q/s640/IMG_20190220_181008.jpg)
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNIsnTrZ5humBnKFmBWkpdW3vvuvWIKHOXb5K6CsjH51ffa80tNjv9eOC9iQkOMP5J7chtuHg5sadmxhIeJd1nH4nB8J9q6DIYYTTvyZHW3CUQ18Q5r2ZLffWtiXGhgY6k0HdJudDyZExy/s640/IMG_20190220_181115.jpg)
Pichani ni baadhi ya wananchi waliohudhuria kwenye kongamano hilo lilifanyika katika hoteli ya New Afrika Jijini Dar es Salaam.
No comments