Breaking News

CUF Wamtaka Maalim Seif aache kuitisha Mahakama.

KYNM kurugenzi wa Habari Bw. Abdul Kambaya 

TAARIFA KWA UMMA
Imetolewa 12/02/2019

CUF-Chama cha Wananchi kinamtaka Maalim Seif Sharif Hamad aache kuitisha Mahakama.

Maalim amekua akinukuliwa kutoa kauli mbalimbali za kuingilia uhuru wa Mahakama kupitia Vikao ambavyo amekua anavifanya katika Visiwa vya Unguja.

Maalim anaitisha Mahakama kua iwapo itahukuhumu kinyume na utashi wake kua atatumia nguvu ya Umma kuonyesha kua hakubaliani na hukumu. 

Maalim aache kuingilia uhuru wa Mahakama kwa kauli zake za vitisho dhidi ya Mahakama, Maalim ameshika nyadhifa mbalimbali kwenye Serikali ya Zanzibar kama vile Waziri Kiongozi na Makamo wa kwanza wa Rais. Ni jambo la aibu kwa Kiongozi alieshika nyadhifa kama hizo kuhuhubiri upotofu dhidi ya Mahakama. 

Maalim anachopaswa kufanya ni kusubiri huku ya mashauri aliyoyafungua na iwapo atashindwa basi anachopaswa kufanya ni kukata rufaa ndio njia za kimahakama na si vitisho eti nitatumia nguvu ya Umma kupinga hukumu hiyo.

CUF-Chama cha Wananchi kinamshangaa Maalim kwanini hakutumia hiyo nguvu ya Umma wakati wa Uchaguzi wa 2015  na badala yake anataka kuitumia wakati huu kama kweli ana nguvu hizo ?

Chuki na hasama anazo jenga dhidi ya Mahakama kupitia Vikao mbalimbali vinavyofanyika Unguja sijambo la kulifumbia macho.

Wito wetu kwa Viongozi wa Vyama vya Siasa kuacha kufanya Vikao kwa lengo la kujenga Chuki dhidi ya Mahakama kwa kiwango hiki kinachonekana sasa kwa malengo tu ya kujenga himaya za Kisiasa.

Tuiache Mahakama itoe hukumu kwa mujibu wa Katiba ya Cuf sambamba na Sheria namba 5 ya Vyama vya Siasa chini ya Sheria mama ya Nchi (KATIBA YA JAMUHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA).

CUF-Chama  Cha Wananchi kina watoa hofu na kuwataka Wanachama wake wote kupuuza vitisho na kebehi za Maalim kupitia Vikao vyake. Tunawaomba mjitokeze kwa wingi kusikiliza hukumu inayotarajiwa kutolewa Tarehe 18-22 ya February na kwa upande wetu tutakubaliana na maamuzi ya Mahakama na kufuata taratibu zitazostahili mara baada ya hukumu.

Ofisi ya Kaimu Katibu Mkuu itaendelea kusimamia majukumu ya kila siku katika itendaji wa shughuli za Chama. 

KYN Abdul Kambaya 
Mkurugenzi wa Habari

No comments