Breaking News

Nabii Richard Godwin Afunguka Tukio La Mtu Kufufuliwa Nchini Afrika Kusini

Wito umetolewa kwa jamii kuacha kubeza au kukashifu tukio ambalo limesababisha sintofahamu kubwa katika jamii mara baada ya kusambaa katika mitandao ya kijamii la kufufuliwa kwa raia mmoja nchini afrika ya Kusini kufatia kuripoti kufariki siku nne kabla ya kuletwa kufanyiwa maombi na mchungaji wa kanisa la Aleluia Ministry Lililopo nchini Afrika kusini.

Akitoa ufafanuzi wa tukio hilo jijini Dar es Salaam nabii wa huduma ya kiroho kutoka katika kanisa la Jehova Mercy Ministry Nabii Richard Godwin alisema tukio hilo ambalo limesababisha sintofahamu tangu kuripotiwa siku ya Jumapili feb 24 kwa mtizamo wake alitakiwi kubezwa wala kuaminiwa kutokana na maandiko namna lilivyotokea.

"Nimekuwa nikipokea simu, ujumbe wa msg kutoka kwa watu mbalimbali waliokuwa wanataka kusikia kauli yake juu ya tukio hilo niseme kwamba kwa mujibu wa maandiko matakatifu na matendo ambayo yamendikwa katika vitabu vitakatifu juu ya kuwepo kwa tukio kama hili ambalo ni kufa na kufufuka kwa bwana yesu pamoja na kitendo cha yesu kufufua mfu ki imani awezi kulibeza wala kukibali juu ya tukio hili." Alisema Nabii Godwin.

Alisema kitendo cha kubeza tukio hilo sio vyema kutokana na kuwepo kwa matukio kama haya ambayo yatambuliwa na vitabu vitakatifu ivyo basi ipo hakuna sababu yeyote ya msingi ya kuanza kubeza tukio hilo badala yake kungoja zaidi taarifa kutoka vyanzo vingine ambavyo ndivyo uwa vinatoa udhibitisho kuwa mtu amefariki kama ripoti ya daktari, ndugu wa karibu na majirani.

"Kwa namna tukio husika lilivyoripotiwa na vyombo vya habari siwezi kusema kama tukuio hilo ni la kweli au si la kweli ila kwa mujibu wa vitabu vitakatifu tukio hilo sio la kwanza kutokea ila nitoe rai kwa jamii kuacha kukashifu na kubeza tukio hilo wakati tukingoja taarifa nyingine kutoka katika taasisi husika" Aliongeza Nabii Godwin.

No comments