Breaking News

TMA Yaendesha Warsha Kwa Waandishi Wa Habari Kuelekea Msimu Mvua Mwezi Machi Hadi Mei Jijini Dar.

Kaimu Mkurugenzi wa mamlaka ya Hali ya Hewa TMA Dk. Ladslaus Chang’a akifafanua jambo wakati wa ufunguzi warsha kwa waandishi wa habari habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM). inayofanyika Shule ya Sheria Ubungo jijini Dar es salaam. 
Bw. Elias Mpiki akiwasilisha mada katika warsha kwa waandishi wa habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM). inayofanyika Shule ya Sheria Ubungo jijini Dar es Salaam. 

Dar es salaam:
MAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendesha warsha kwa waandishi wa habari habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dk Agness Kijanazi Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Ladslaus Chang’a alisema warsha hiyo muhimu inalenga kujadili mwelekeo wa msimu wa mvua na kufanya tathmini ili kuboresha zaidi taarifa za utabiri.

Alisema TMA itaendelea kutoa elimu kwa wanahabari kwani ni kiungo na wadau muhimu katika utoaji na usambazaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa nchini.

“Naomba mtambue kuwa wanahabari ni kiungo muhimu cha usambazaji wa taarifa zetu na tunathamini sana michango yenu ndio maana tunawashirikisha…,” alisema Chang’a akifungua warsha hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agnes Kijazi.

Aidha aliwaomba wanahabari kuzingatia warsha wanazopata kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini na kuwa mabalozi wazuri wa taasisi hiyo katika kuuelimisha umma juu ya umuhimu wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa.
Baadhi ya maofisa kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa wakifatilia mada zilizokuwa zikiwasilishwa katika warsha ya waandishi wa habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM). inayofanyika Shule ya Sheria Ubungo jijini Dar es salaam.

Baadhi ya waandishi wa habari walioshiriki katika warsha ya waandishi wa habari kwa ajili ya maandalizi ya kupokea utabiri wa msimu wa mvua wa mwezi Machi hadi mwezi Mai 2019 (MAM). inayofanyika Shule ya Sheria Ubungo jijini Dar es salaam.

No comments