Breaking News

Ubalozi Wa Swiden Wasaini Makubaliano Ya Ushirikiano Na LHCR, Na kuzindua Mpango Mkakati Wa Kipindi Cha Miaka 6.

kituo cha sheria na Haki za binadamu na Ubalozi wa Uswidi (Sweden) wamesaini makubaliano ya ushirikiano utakaojumuisha mipango na mkakati wa taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka 6 kuanzia 2019 hadi 2024.

Akizungumza mapema mara baada ya kusaini makubaliano hayo jijini Dar es Salaam mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Bi. Anna Henga alisema serikali ya Uswisi kupitia ubalozi wake hapa nchini wamekuwa wahisani kwa muda mrefu katika kufadhili miradi ya maendeleo yenye lengo la kuleta mabadiliko chanya kudumisha ulinzi wa haki za binadamu na utawala wa sheria.

"Serikali ya Uswisi kupitia ubalozi wake nchini wamekuwa wahisani wetu kwa mda mrefu tangu mwaka 2001, pia wamekuwa marafiki wa mda mrefu wa serikali ya Tanzania kwa kujikita kufadhili miradi mbalimbali ya maendeleo itakayoleta mabadiliko chanya katika kupinga umasikini, kuchagiza maendeleo, kudumisha demokrasia na ulinzi wa haki za binadamu nchini" Alisema Bi Henga.
Alisema kupitia makubaliano hayo kituo cha sheria na Haki za binadamu litaweza kufikia malengo yake kwa kuifikia jamii yenye Haki na usawa kwa kuandaa na kutekeleza malengo mkakati ya kuratibu ya kuratibu kazi zao za utetezi wa haki za binadamu katika kipindi cha miaka sita ya makubaliano hayo.

Ameyataja malengo hayo kuwa ni pamoja na kujengea umma uwezo juu ya haki za binadamu, kufanya uchambuzi kwa lengo la kuboresha au kubadilisha sheria, kupanua ushiriki wa wananchi, kukuza na demokrasia pamoja na kuchochea mabadiliko ya katiba.

Bi Henga ametaja mengine kuwa ni kudumisha haki za kijamii pamoja na kiuchumi, kuhakikisha kila mwananchi anapata haki ya kuishi katika mazingira safi na salama zinazingatia, kuboresha sheria na sera zinazosimamia haki za wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

No comments