Breaking News

TAKUKURU Mkoa wa Temeke Yaokoa Zaidi Ya Mil 36.

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoa wa Temeke imesema katika kipindi cha mwezi Oktoba hadi Disemba mwaka jana imefanikiwa kuokoa zaidi ya Mil 36 kutokana na kupambana na mianya ya rushwa huku ikibainisha dawati la uchunguzi kupokea taarifa 130.


Akizungumza Jijini Dar es Salaam na Naibu Mkuu wa Takukuru, Ramadhan Ndwatah wakati akitoa taarifa za utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo katika kipindi cha miezi hiyo.

Amesema kuwa dawati la uchunguzi lilifanya kazi kubwa ya kuhakikisha vitendo vya rushwa vinapungua mkoa wa Temeke kwa kuziba na kupambana na mianya ya rushwa na kubainisha kuna kesi tisa zinazoendelea mahakamani.

“ Dawati limefanya jitihada za dhati kuhakikisha fedha zinaokolewa hata hivyo majalada mapya uchunguzi 15 yaliyofunguliwa yamepokelewa,” Alisema Bw. Ramadhan.

Amebainisha kuwa katika kipindi hicho dawati la elimu kwa umma limetekeleza majukumu yake kwa kupitia semina 14, makala moja, mikutano  miwili na vyombo vya habari, mikutano ya hadhara 18 na kwamba wananchi walioelimishwa ni 6402.

Amefafanua kuwa  dawati la utafiti na udhibiti la mkoa huo limefuatilia miradi mine iliyokamilika kwa asilimia mia ikiwemo ya mradi wa ujenzi wa miundo ya maji Mtaa wa Mkonongwa-Chamazi wenye thamani ya Sh Bilioni 1.9 Mradi wa  ujenzi wa wodi ya wazazi ,maabara na chumba kuhifadhia maiti na chumba cha upasuaji kituo cha Afya Kigamboni Sh Bilioni 4, pamoja na ujenzi wa Jengo la ghorofa mbili Shule ya Sekondari Kigamboni Awamu ya kwanza ukiwa na thamani ya zaidi ya mil 93.

Katika hatua nyingine, amesema wana malengo na mikakati kuendelea kufanyia kazi malalamiko yote ya rushwa kwa wakati na weledi, kuendelea kutoa wito kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa kufichua vitendo vya rushwa pamoja na kutoa elimu ya mapambano ya rushwa na utawala bora katika maeneo yanayolalamikiwa. 

No comments