Breaking News

TIC Yaunga Mkono hatua ya Rais Magufuli kuhamishiwa Ofisi ya Waziri Mkuu na kupewa wizara kamili

Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geofrey Mwambe wakati akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) makao makuu jijini Dar es Salaam. 

Na Hussein Ndubikile. Dar es Salaam
Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesema kinampongeza na kufurahishwa na hatua ya Rais DKT John  Magufuli  kwa kufanya uamuzi ya kuanzisha Wizara inayoshughulikia masuala ya uwekezaji, tofauti na awali ambapo shughuli zote za kituo hicho  zilikuwa zikifanyika chini ya Wizara ya Viwanda,Biashara  na Uwekezaji.

Aidha kituo hicho, kimesema kimefurahishwa na hatua ya Rais Magufuli kumteua, Angellah Kairuki kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Uwekezaji na kubainisha kuwa kufanya hivyo kutachangia kwa kiasi kikubwa kutelekeza majukumu yake ipasavyo hasahasa kwenye masuala ya uwekezaji.  

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Geofrey Mwambe wakati akizungumza na wanahabari ambapo amesema kitendo cha kituo kupewa Waziri kamili na katibu wake kutarahisisha utekelezaji wa mipango na majukumu yake ikiwemo kuendelea kuvutia wawekezaj wa ndani na nje, kutengeneza mazingira rafiki ya uwekezaji na kuandaa namna bora ya kujadili masuala ya uwekezaji.

Amebainisha kuwa kituo hicho kina umuhimu katika kujenga uchumi wa nchi kupitia uwekezaji na kwamba  na kwamba anaamini uwepo wa viongozi ni chachu ya nchi kuelekea uchumi wa kati kupitia uwekezaji wa viwanda.

Mwambe ametoa wito  kwa taasisi binafsi, taasisi za Serikalipamoja na  serikali za mitaa kuendelelea kushirikiana na TIC katika kuibua fursa na kutangaza fursa za uwekezaji ndani na nje ya nchi.

"Jana niliongea Waziri wa Fedha na Mipango, alitusisitiza tujitahidi sana kujenga mazingira ya uwekezaji na yawe rafiki zaidi asiwepo mtu wa kukwepa kulipa kodi na tukifanya hivyo tutamsaidia sana Rais na wawekezaji waendelee kuiona Tanzania kuwa nchi salama katika uwekezaji, " amesema Mwambe.

Amezitaka taasisi binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali, kushiriki kikamilifu katika kutangaza fursa za uwekezaji huku akibainisha kuwa hali ya uwekezaji Duniani mwaka 2018,  ilishuka kwa 23%  kwa Afrika Mashariki Tanzania  ilipata Dola za kimarekani  billion 1.365 mwaka 2017,mwaka 2018 ilishuka hadi dola za kimarekani  billion 1.2  lakini iliongoza  Afrika Mashariki na kufanya vizuri kimataifa.

Katika hatua nyingine, amesema amesikitshwa na kitendo cha Kitendo cha Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kutoonyesha uzalendo wakati akihojiwa na kituo cha Televisheni cha nje ambapo alisikika akitamka maneno ya kuibomoa nchi.

"Nimeona clip ya Tundu Lissu akihojiwa na kituo cha televisheni huko nje ya nchi, huo siyo uzalendo  inaonekana Mtangazaji  anajua zaidi anaipenda Tanzania kuliko yeye, nimemshangaa  sana ,anaibomoa nchi wakati yeye ndiyo anasema anataka kugombea 2020"amesema.

Mwambe ameishukuru Serikali kwa kuiongezea TIC watumishi na Mikoa iliyotenga maeneo ya Uwekezaji ukiwemo mkoa wa Pwani na Kigoma.

No comments