Breaking News

CUF kufanya Dua Kesho, Kuwakumbuka Waanga Wa Maandamano Ya Amani Ya Tarehe 26/27 Mwaka 2001.

Chama cha wananchi CUF kesho tarehe 27
watafanya dua ya kuwakumbuka wahanga waliopoteza maisha katika maadamano ya amani yaliyoandaliwa na chama hicho mwaka 2001 katika miji ya Dar es Salaam, Pemba na Unguja. 

Akizungumza mapema leo jiji dar es salaam mwenyekiti wa taifa wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba alisema katika kuadhimisha na kuwakumbuka watanzania hao zaidi ya 70 ambao walipoteza maisha ofisi zote za CUF nchi nzima bendera zitapepea nusu mlingoti. 

"Katika kuwakumbuka na kuwaenzi wale wote waliopoteza maisha na walipata ulemavu katika maandamano hayo ya amani chama cha wanachi CUF kimeandaa dua ya kuwaombea ambayo kitaifa itafanyika mkoani Dar es Salaam katika kata ya Mnyamani" Alisema Profesa Lipumba. 

Akielezea tukio hilo profesa Lipumba alisema siku ya tarehe 26/27 Januari 2001 wanachama wa chama hicho pamoja na kujua mwenyekiti wao anashikiliwa na jeshi la polisi waliojitokeza kwa wingi kushiriki maandamano ya amani mara baada ya kumalizika kwa swala ya Ijumaa. 

Alisema mara baada swala jeshi la polisi walifika kujaribu kuwatawanya kwa kuanza kuvyatua risasi za moto kitendo kilichopelekea kupeteza maisha kwa watanzania 70 wengi wao wakiwa wanatoka kisiwa cha Pemba na Unguja na wawili kutoka Dar es Salaam. 

Akiongelea chanzo cha chama hicho kuitisha maandamano hayo ya amani nchini nzima profesa Lipumba alisema maandamano hayo ya amani ni kutoa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kutekeleza mambo manne waliokuwa wakiyapigania kwa manufaa ya taifa. 

Ameyataja mambo hayo kuwa ni kuanzishwa mchakato wa katiba mpya, tume ya uchaguzi, kurejewa kwa uchaguzi wa Zanzibar pamoja na kuwepo na utawala bora unaoheshimu haki za binadamu nchini. 

No comments