Breaking News

Mchungaji Mashimo Amtaka CAG Kuwaomba Radhi Bunge Na Watanzania Kwa Kauli Yake.

Mchungaji wa Manabii na Mitume Komando Mashimo amemtaka dhibiti na mkaguzi wa hesabu za serikali nchini Prof Mussa Assad kuomba radhi kwa Bunge na watanzania Kufatia kauli aliyoitoa wakati akiojiwa na radio moja nje ya nchi na kusema bunge ni dhaifu ni aibu kubwa sana kwa kiongozi huyo wa umma

Akizungumza jijini dar es Salaam mchungaji mashimo alisema kauli hiyo pamoja na kuvunja heshima ya serikali na watanzania namtaka kutafakali kiongozi huyokutafakali kwa kina pamoja na kuomba radhi kwa bunge pamoja na watanzania wote.

"Nitoe rai kwa mkaguzi na mdhibiti wa hesabu za serikali kuomba radhi bunge pamoja na watanzania kwa ujumla kwani kauli aliyoitoa inaonyesha kuwa viongozi wote wa serikali yote awafai na kuaribu taswila ya taifa kimataifa" Alisema Mchungaji Mashimo.

Aidha mchungaji mashimo amemtaka kiongozi huyo kufanya toba kutokana kauli alioitoa na kupelekea kuibuka kwa malumbano kutokana katika jamii hivyo kushauri busara kutumike katika kulitatua swala hilo.

"Bunge ni sehemu tukufu hiyo maneno yaliotamka profesa....yamepelekea chombo hicho kitukufu kukikosea heshima na ikizingatiwa kauli yake ameitoa akiwa nje ya nchi" Alisema. 

No comments