Mchungaji MASHIMO: Atoa Maono Amtaka Waziri Asietenda Haki kufanya Toba.
![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjGi7GDT3LPlVtZN0Mgwrb8FO3LGlQwoxmqs7EPRCP8id2DXl8FdFX_iXd1gNcXORrbUzyC6KcaZpXSZi9vP9KjqCL2s1Jmjio5U-E8fCM5yoQeDLi9BaLx1lNvKFEMegb0Dc2PGzjCUIAX/s640/IMG_20190107_101145.jpg)
MCHUNGAJI wa Mitume, Manabii na Maaskofu Tanzania Komando Mashimo, ameelezea maono yake kwa mwaka huu wa 2019 kwa kumtaka mmoja wa mawaziri wa serikali ya Awamu ya Tano kufanya Toba kwa ubaya alioutenda dhidi ya moja ya familia kabla ya kukutwa na mauti.
Akizungumza jijini Dar es Salaam alisema maono ya unabii wa vifo na vilio kwa watumishi wa umma na Mawaziri ambayo ameonesha na Mungu wake ambaye ni Mungu wa kweli kuwa kutatokea kutokea vifo hususani kwa Waziri mmoja wa serikali ya awamu ya tano.
Kwa mujibu wa maono hayo, Mchungaji Mashimo alidai kuwa tukio hilo limetokea katika Mikoa ya Kusini na kwamba waziri huyo alitenda unyama huo dhidi ya mtu ambaye awali kabla ya kupata wadhifa huo wa uwaziri walikuwa wakishirikiana na hivyo kuacha familia ya mtendwa wa uovu huo ikilia.
Aliendelea kufafanua kua moja ya ubaya alioutenda dhidi ya mtu huyo ni kumdhrumu mali na kumuacha yeye na familia yake katika dimbwi la masikitiko wasijue lakufanya.
“Ipo familia inalia, familia imetendwa jeuri, Mungu akanipa picha zaidi nikaona askari wakiwa na mitutu ya bunduki na mtu mmoja mwembamba ni kamuuliza Mungu huyu mtu ni nani, alisindikizwa hadi ndani ya benki huku nje kukiwa na askari wenye mitutu,” alisema Mashimo.
“Baada ya muda kidogo akatoka ndani ya benki akakabidhi fedha, nikamuuliza Mungu nini maana na ndoto hii akasema yupo mwanasiasa mmoja ambaye amefanya jambo hili, jambo hili limetokea mikoa ya kusini,” alieleza.
Mchungaji Mashimo alisema kuwa kama kiongozi huyo asipofanya toba atakutwa na mauti pamoja na watu aliowatumia katika kutenda uonevu huo.
“Kuna watu watakinywea kikombe hiki wasipofanya toba na kuifata familia ile kuiomba msamaha kwani Mungu atawapiga,” alisema..
Aidha alisema wakati hayo yote yakitendeka Maono yanaonesha kuwa hadi sasa jambo hilo bado halijamfikia Rais John Magufuli.
Hata hivyo katika Maono hayo Mchngaji Mashimo hakuweza kumtaja waziri huyo wala familia iliyotendewa ubaya kwa madai kuwa Mungu hakumbainishia hayo.
Alitoa wito kwa kuwataka viongozi wa Umma na Serikali katika ngazi mbali mbali kumsaidia Rais Magufuli kwa kuwahudumia wananchi kwa kuwatendea haki.
“Ni jambo jema viongozi wa umma kutenda haki katika majukumu yao, kitu ambacho kitasaidia kuleta maendeleo,” alisema.
No comments