Breaking News

Dkt Shika Kuja Na Project Hizi Kufunga Mwaka 2018

Bilionea wa Nyumba za Lugumi na Rais wa Kampuni ya Ralcefort ya nchini Urusi Dk. Luis Shika amesema ana mpango wa  kujenga kiwanda cha  kutengeneza taulo za kike mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Dk. Shika alisema ujenzi wa kiwanda hicho ambacho uratibu wake umeshaanza ni zawadi kwa wanawake kuelekea sikukuu za Krisimasi na mwaka mpya na taulo hizo zitakuwa zikitawanywa bure.

“Natajia kutoa kama zawadi ya Krismasi na mwaka mpya zawadi ya kiwanda cha kutengeneza taulo za kike bure na kuzitawanywa kwa wahitaji kote Duniani,” alisema Dk. Shika.

Alisema kiwanda hicho kitajengwa na kampuni ya Kijapani na tayali kazi ya usanifu wa awali na uchoraji wa ramani ya kiwanda hicho umeanza hili ujenzi uanze mara moja kwani fedha zote za kugharamia ujenzi huo zipo. 

"Najua jamii itakuwa na sintofahamu juu ya uhamuzi wa kuwapa wajapani kujenga kiwanda hicho nmechukua uhamuzi huu kutokana na fedha zake kuwa nchini Japani hivyo itakuwa rahisi kuwalipa.
Katika hatua nyingine Dk. Shika amemtambulisha Msanii Chipukizi wa Muziki wa Kizazi Kipya maarufu kama ‘Bongo fleva’ Salim Magembe ‘K.L.O.H’ ambaye atakuwa chini yake. 

Kama mtakumbuka nimekuwa nkisapoti wasanii mbalimbali na kusimamia kazi zao nchini kutokana na kuwa na vipaji, sauti nzuri, uwezo mzuri wa kuimba na mwonekano wa kisanii.

Msanii niliyemsainisha leo amekizi vigezo vyote kuwa msanii kutokana na kuwa na uwezo mzuri wa kutunga mashairi yenye kuendana na rika mbalimbali pamoja na kuwa na maadili.

Kwa upande wake Msanii huyo alisema kuwa hadi sasa tayali amesharekodi nyimbo za audio zaidi ya 30 na video mbili ambapo miungoni mwa nyimbo hizo amewashirikisha wasanii wakongwe kama P.N.C na Country Boy.

“Mimi ni msanii chipukizi niliyeanza muziki miaka miwili iliyopita na nimeweza kufanya kazi kadhaa, nina audio zaidi ya 30 na video mbili, video moja nilifanya mwaka jana niliyomshirikisha P.N.C lakini haikuweza kufika popote kutokana na kokusa fedha,” alisema Magembe.

No comments