Dc MATIRO Atinga Kata Ya Wakata Mapanga ,Apigisha Kura Za Siri Kubaini Wauaji

Kufuatia kuibuka
kwa taarifa za kuwepo kwa mauaji ya wanawake yanayoambatana na imani za
kishirikina katika kata ya Salawe wilaya ya Shinyanga, mkuu wa wilaya hiyo
Josephine Matiro amefanya mkutano na wananchi wa eneo hilo kwa ajili ya
kutafuta chanzo na ufumbuzi kumaliza mauaji hayo.
Wananchi wa kijiji
cha Songambele kata ya Salawe wanasema mauaji hayo yameanza kutokea tangu mwezi
Desemba mwaka jana wakidai kuwa wanawake hukatwa mapanga ama kunyongwa na watu
wasiofahamika ambao hutoweka na viungo vya siri vya wanawake wanaowaua.
Inaelezwa kuwa katika kipindi cha Januari Mosi hadi Machi 23 mwaka huu watu waliouawa katika kata hiyo ni wanne huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za kishirikina.
Inaelezwa kuwa katika kipindi cha Januari Mosi hadi Machi 23 mwaka huu watu waliouawa katika kata hiyo ni wanne huku mauaji hayo yakihusishwa na imani za kishirikina.
Kutokana na hali
hiyo Mkuu wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro ambaye ni mwenyekiti wa kamati
ya ulinzi na usalama wilaya hiyo, alifika katika kata ya Salawe kwa ajili ya
kutafuta ufumbuzi wa mauaji hayo kwa njia ya kuwashirikisha wananchi.
Aidha baada ya
kuzungumza na wananchi wa eneo hilo katika mkutano wa hadhara,mkuu huyo wa
wilaya aliagiza kufanyika/kupigwa kwa kura za maoni kwa ajili ya kuwabaini
wahusika wa mauaji hayo na kuondoka na kura hizo kwa ajili ya kuzifanyia kazi.
“Katika wilaya ya Shinyanga kuna kata 43, matukio ya mauaji ya namna
hii yanatokea hapa,ni nyinyi hapa tu,sasa tumtafute mchawi na tumfanyie
kazi,mkitaka kulimaliza tatizo hili ni lazima mtupe ushirikiano,muwe
tayari kufika mahakamani pale mtakapohitajika ,mjitokeze kutoa ushahidi ili
wale watu msiwaone tena kwenye mitaa yenu”,alisema Matiro.
“Wananchi mmeendelea kulalamika kuwa kuna mauaji na kuitupia lawama
serikali wakiwemo askari polisi kuwa wanapokea rushwa na kuwaachia huru
watuhumiwa kumbe tatizo ni nyinyi kutotoa ushirikiano,naomba mbadilike,
wafichueni wahusika ili tukomeshe tatizo hili kwani tunataka watu wawe salama
na waishi kwa amani”,alieleza Matiro.
Aidha aliwataka
viongozi wa serikali za mitaa na wananchi kwa ujumla kuacha kupokea wageni na
kwamba wageni wote wajitambulishe ili kujua wanafanya nini na wametoka wapi ili
kukomesha
Wakizungumza mbele
ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga, wananchi hao walisema matukio hayo yanatishia
usalama wao na kusababisha waishi kwa hofu.
Walisema mbali na
kuishi kwa hofu pia wanashindwa kufanya kazi zao za maendeleo na uzalishaji
mali.
Kwa mujibu wa
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, ACP Simon Haule aliyekiri kuwepo kwa
mauaji katika kata ya Salawe alisema chanzo ni kuwania mali,migogoro ya
mashamba,wivu wa mapenzi na imani za kishirikina.
Aidha aliwataka
wananchi kupuuza uzushi kwamba kwenye kata hiyo kuwa kuna watu wanakata mapanga
wanawake na kisha kuondoka na sehemu zao nyeti yakiwemo matiti.
“Kwenye mkoa wa
Shinyanga hakuna kitu kama hicho, isipokuwa kuna takwimu za wananchi 27 kuuawa
kwa kukatwa mapanga kutokana na sababu mbalimbali kwa kipindi cha miaka mitatu
mfululizo kuanzia (2016- Machi 2018) ambapo wanawake 12, na wanaume 15.
Alitaja takwimu za
mauaji mkoa wa Shinyanga kwa kuchambua kila mwaka ambapo mwaka (2016) waliuawa
watu 12, wanawake Sita, Wanaume Sita, (2017) wanaume nane, wanawake wanne,
mwaka huu (2018) kuanzia Januari hadi Machi wanawake wawili na mwanaume mmoja
jumla watu 27.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza na wananchi wa kijiji cha Songambele kata ya Salawe kwa ajili ya kutafuta mwarobaini wa kumaliza tatizo la mauaji katika eneo hilo

Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.




Wananchi wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Shinyanga
Picha Na Stephen Wang'anyi - Malunde1
No comments