STARTIMES Yamkutanisha Staa Wa Uigizaji Kutoka Nchini China Na Wasanii Wa Filamu Nchini.
Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing
"Mau Dou Dou" (kushoto) akizungumza jambo kwenye mkutano na
waandishi wa habari, wasanii wa filamu nchini pamoja na mashabiki wake Jijini
Dar es Salaam
Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Zuhura
Hanif (kulia) akimkabidhi tuzo Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing
"Mau Dou Dou" (kushoto) kwa niaba ya watanzania ambao ni
mashabiki wake
Msanii wa filamu nchini Tanzania, Suzan Lewis
"Natasha "(kulia) akitoa shukrani kwa niaba ya wasanii wa filamu nchini
wakati wa ziara ya Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing
"Mau Dou Dou" alipofika na kufanya mazungumzo nao jijini Dar es
Salaam.
Baadhi ya wasanii wa Filamu nchini pamoja na
mashabiki wa Mwigizaji maarufu wa China, Hai Qing "Mau Dou
Dou" wakifuatilia mada wakati wa mkutano huo katika ukumbi wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
Kampuni ya STAR MEDIA (T) Ltd kupitia bidhaa yake ya
StarTimes imewakutanisha muigizaji maarufu wa China Hai Qing maarufu kama
Mau Dou Dou na wasanii wa Kitanzania pamoja na mashabiki wake kwa lengo la
kujadilishana Uzoefu katika Sanaa za Uigizaji.
Hafla hiyo ya
kuwakutanisha wasanii hao imefanyika leo Jijini Dar es Salaam,katika
ukumbi wa kimataifa wa Mikutano wa Mwalimu Nyerere (NICC) na kuhudhuriwa na
wasanii mbalimbali maarufu, pamoja na waandishi wa habari.
Mwigizaji
huyu wa Kimataifa kutoka nchini China, Hai Qing maarufu kama Mau Dou
Dou ambaye atakuwepo nchini Tanzania kwa ziara ya siku mbili pamoja na mambo
mengine imejikita kubadilishana uzoefu na waigizani wa hapa nchini sambamba na kutangaza kampuni ya Startimes.
Akizungumzia
ujio huo wa Mau Dou Dou, Makamu wa Rais wa Startimes Tanzania, Bi. Zuhura Hanif
alisema msanii huyo ni mja ya waigizaji wakubwa anatangaza lugha ya Kiswahili kupitia king’amuzi cha Startimes.
Alisema
Kampuni ya kampuni ya StarTimes inatumbua mchango wa Lugha ya Kiswahili katika mawasiliano msanii huyo atakuwa na kazi nyingi kwa kushirikiana Ubalozi wa nchini China pamoja na
Startimes lengo likiwa ni kukuza Kiswahili.
Halfa
hiyo meduliwa na ambayo wasanii mbali mbali wakiwemo Natasha, Yvone na
Davina.
No comments